Papaa Mobimba
JF-Expert Member
- Jan 27, 2018
- 882
- 3,337
Chama Cha Mapinduzi kimesema kwamba uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024 utatuma salama kwa mtu au chama chochote kinachotaka kupambana na Rais Samia Suluhu Hassan mwaka 2025 huku kikidai kuwa atakeyetaka kuthubutu ajitafakari upya kama ana sifa za kupambana.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Mkoa wa Dodoma, Jawadu Mohammed alipokuwa akiwanadi wagombea wa nafasi za uenyekiti na ujumbe wa Serikali za mitaa, vitongoji na vijiji katika kijiji cha Keikei kata ya Keikei wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma.
Aidha amesema baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuachiwa nchi na Hayati Dkt. John Pombe Magufuli watu wengi pamoja na baadhi ya vyama vya siasa walidhani Rais Samia hatoweza kuongoza nchi lakini imekuwa tofauti kwani ametekeleza miradi ya maendeleo kwa kiasi kikubwa.
Jambo TV