JB: Wasomi wa Tanzania ni vilaza, afadhali ya sisi wasanii tusiosoma

Interest

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2015
Posts
3,434
Reaction score
7,072
Muigizaji na muongozaji wa filamu, Jacob Stephen aka JB amesema amesikitishwa na mfumo wa elimu ya Tanzania baada ya kushindwa kumpata mtanzania wa kushika nafasi ya masoko kwenye kampuni mpya aliyoingiza hisa zake na nafasi hiyo kuchukuliwa na raia wa Kenya aliyeonyesha uwezo mkubwa kuliko Watanzania waliokuwa wakiwania nafasi moja.

Haya nimekutana nayo wakati niikiperuzi kwenye akaunti yake ya mtandao wa Instagram;

Jana nimesikitika sana…kuna kampuni mpya ambayo na mimi nina hisa zangu chache na wazungu fulani (nitaitangaza baadae) ilikuwa inataka watu wa masoko…dah mmh watu karibu 10 kwenye usahili. Wana madigree yao hawana mbinu mpya za kuingiza bidhaa hiyo sokoni, kaja mkenya kashinda, hivi elimu yetu inatuandaa kuwa tutakapomaliza tuwe chini ya mabosi tutakaowakuta kazini. elimu gani hiyo inashindwa kuikomboa jamii inayokuzunguka. elimu isiyoweza kuajiri hata watu 5. angalia hata kwenye fani zetu uigizaji, mziki, watangazaji hata waandishi wasomi wengi hawapo na watu wanafanya vizuri. ingawa sasa tunahitaji mbinu mpya toka kwao. mzungu alichukia akasema machinga wana mbinu mpya kuliko hawa…akosee mtu kizungu utawaona heee wasanii hawajasoma…jiulize elimu yako imelisaidia nn taifa. sisi wengi wetu ni form4 lakini tumetoa ajira kubwa kwa watu. wasanii, liabrary, machinga, maduka mengi tu ingawa tuna mapungufu mengi. wasomi njooni tusaidiane huku pia kuna pesa amkeni.

Mimi nimemwelewa na namuunga mkono, nani ana hoja mbadala?

Nawasilisha..

 
Yupo sahihi. Kibaya zaidi ukimpa mtu kazi ya marketing anaanza longolongo za kutouza na kuja na excuses kibao. Inashangaza mtu wa marketing anafocus kwenye mshahara mwisho wa mwezi badala ya commission kwa mauzo atakayofanya. Hongera sana JB kutuchana sisi wasomi.
 
Yeye binafsi ana nini cha kujivunia labda?
 
Point anayo! Ingawa nimemind kupondwa na kadigirii kangu...
 
That's right. JB got a point, our education is going worse; most of the graduates lacks confidence, creativity, & self independence spirit. All of these are resulted from our poor traditional & theory based education( education which put emphasis on less competence &practices).
 
Ni aibu sana...Elimu ya Kudesa kupata vyeti..
 
Waliokimbia shule wanapondea waliosoma .....huyo JB ana kampuni gani ya kujivunia movie zenyewe ana copy za kihindi
 
Kiukweli elimu tuliyonayo au tunayoipata vyuoni inatutosha haina tatizo lolote lile mwenye tatizo ni mwanafunzi tu mwenyewe maana yeye ndo mwenye mtazamo either aajiriwe au ajiajiri kwa elimu aliyonayo...kama unabisha wabongo wengi tunatatizo tunapenda sana kuajiriwa compare profiles za wabongo wengi linked in na za wahindi wa bongo huko linked in utajionea na pia maana mtu anaexperience ya miaka 10 kwenye marketing lakini hana hata professional company yakufanya marketing
 
Hamna lolote ambaye hajasoma hawezi kujilinganisha na msomi hata kidogo.elimu yetu inatusaidia sana tuu..wengi wamefika mbalii.chukua maisha ya ambao hawajaenda shule na walioenda shule angalia ni wapi kwa asilimia kubwa wana ganga njaa au kusulubika sana ndo wapate ahueni..waende shulee
 
JB kaongea kweli tupu ni aibu asee wasomi wengi tumeshakua addicted na haya mamitandao, from sunrise to sunset hakuna challenge yoyote. Halafu bora ukute tunatumia in a useful way, ni umbea tu na ku upload mapicha muda unaenda adi tunazeekea home sema wazazi wanakausha tu. Ila tubadilike watz.

My take: masomo ya entrepreneurship yawekwe kwenye kila course haijalishi ni course gani sio chuo tu kuanzia secondary level.
 
Waliokimbia shule wanapondea waliosoma .....huyo JB ana kampuni gani ya kujivunia movie zenyewe ana copy za kihindi

Tatizo la watanzania hatutaki challenges kabisa na akili zetu hazikubali kwamba mtu mwenye elimu ya kawaida anaweza kumshauri mwenye elimu ya chuo kikuu,ujinga wa hali ya juu sana.
Ukweli ni kwamba watu wana degree ndio but just on the papers,binafsi hapa ninapopatia mkate wa kila siku nimepewa authority to hire and fire,kiukweli kuna watu hapa wanakuja ku-apply lakini vichwani ni totally empty,hata ukijitahidi umpe probation ili umtizame lakini deliverance still ni below 30%.
Watz tubadilike,tusisome kufaulu mitihani tu.
 
Kama wasomi wetu ndio aina ya Chenge, aina ya Lissu, aina ya Lipumba, basi namuunga mkono 100%. Elimu yetu haina maana kabisa
 
Akumbuke hata yeye kupata hivyo vijisenti ni kwa sababu ya wingi wa vilaza bongo, otherwise wenye elimu gani wangeangalia hayo mauzauza yao ya bonge muvi ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…