Pre GE2025 Je, 2025 Kassim Majaliwa atagombea Ubunge?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Idofu

Senior Member
Joined
Oct 24, 2022
Posts
116
Reaction score
199
1728988512884.jpeg

Nauliza tu kwa wabobevu wa siasa je, 2025 Mh. Waziri Mkuu atagombea tena Ubunge?

Na kama atagombea na Mh .Rais akamteua mtu mwingine kuwa Waziri Mkuu, hadhi yake itakuwaje Bungeni?
 
Angekua anajitambua angegombea Urais hata kupitia CCM au aanzishe chama, ila kwa kuwa hajitambui atagombea ubunge akisubiri "fadhila" apewe teuzi.
Kwahiyo Mzee Lowassa alikuwa anajitambua alipogombea 2015 kupitiwa Chadema? Na kwanini alirudi CCM?
 
Kujitambua means either unaenda one step above au unaachia race sio unasubiri huruma za mtu ndio aokoe political career yako.

Kama Ndugai hakua na option zaidi ya either kumface Samia 2025 au astaafu but he chose the latter lolote other than that atapotezwa kisiasa kabisa.

Na hii iende kwa Kabudi, Lukuvi, Bashiru and the likes, kusubiri huruma za teuzi ni kheri kustaafu tu.
 
Nauliza tu kwa wabobevu wa siasa! Je 2025 Mh.Waziri Mkuu atagombea tena Ubunge?

Na Kama atagombea na Mh.Rais akamteua mtu mwingine kuwa Waziri Mkuu,hadhi yake itakuwaje Bungeni?
Haijawahi tokea Waziri Mkuu Kwa miaka 10 agombee Ubunge Ili avumbue nini?

Hata asipogombea anapata 80% ya Stahiki za Waziri Mkuu wa wakati huo,hakuna Dalili za njaa.

Mwisho atakuwa na Vyeo vingi tuu ikiwemo kuwa Mkuu wa Chuo au nafasi zozote ambazo atapata ,kwani umewahi kuona Pinda anakosa jukwaa?

Anaweza kuja kumrithi Kinana vile vile
 
Namshangaa aliyesema eti "Ataishije"!
Huyo atakuwa "WAZIRI MKUU MSTAAFU", na kuendeleza ile KUIKAMUA NCHI, kwa kuchuma mafao ya WAZIRI MKUU MSTAAFU!
 
Nauliza tu kwa wabobevu wa siasa! Je 2025 Mh.Waziri Mkuu atagombea tena Ubunge?
Kwa mujibu wa katiba, anaruhusiwa ila kwa utamaduni wa CCM, hagombei tena, huyu ni mtu mkubwa sana.
Na Kama atagombea na Mh.Rais akamteua mtu mwingine kuwa Waziri Mkuu,hadhi yake itakuwaje Bungeni?
Hawezi kuteuliwa tena uwaziri Mkuu, amefikia mwisho kwa mujibu wa katiba.
P
 
Nauliza tu kwa wabobevu wa siasa! Je 2025 Mh.Waziri Mkuu atagombea tena Ubunge?

Na Kama atagombea na Mh.Rais akamteua mtu mwingine kuwa Waziri Mkuu,hadhi yake itakuwaje Bungeni?
Akigombea au asigombeee, itapandisha au kushusha uchumi? Hii ncji imejaa porojo mfu sana Daily ni porojo zisizo kuwa na kichwa wala miguu, si bure tunaendelea kuwanchi ya wachuuzi, kwa akili za kipumhavu kama hizi lazima tuwe wachuuzi.
 
Mi nashauri astaafu tu, ukishafikia cheo cha Waziri Mkuu kinachofata ni kuwa Rais au walau Makamu na sio vinginevyo, haimaanishi kama akitaka kuendelea kuwa mbunge ni uroho wa madaraka au kutoridhika anaweza kuwa na nia thabiti ya kuwaendeleza wananchi wake

Lakini kwa muda alioutumikia hiyo nafasi, nadhani kama taratibu, vigezo na miongozo inaruhusu ni wakati muafaka wa kwenda juu ama sivyo kuachia ngazi kabisa na kuwapisha wengine waendeleze alipoishia
 
Kujitambua means either unaenda one step above au unaachia race sio unasubiri huruma za mtu ndio aokoe political career yako.

Kama Ndugai hakua na option zaidi ya either kumface Samia 2025 au astaafu but he chose the latter lolote other than that atapotezwa kisiasa kabisa.

Na hii iende kwa Kabudi, Lukuvi, Bashiru and the likes, kusubiri huruma za teuzi ni kheri kustaafu tu.
Halafu wanatuambia tuji-ajiri
 
Back
Top Bottom