Pre GE2025 Je, ACT Wazalendo watakubali kushinikiza maboresho ya sheria ya uchaguzi kupitia msimamo wa Chadema?

Pre GE2025 Je, ACT Wazalendo watakubali kushinikiza maboresho ya sheria ya uchaguzi kupitia msimamo wa Chadema?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Ni kweli kwamba sheria ya sasa ya uchaguzi ni kwaajili ya CCM siyo kwa ajili ya umma. Sheria imetengenezwa kumzuia hata mwana CCM aliyetakiwa na chama ila anatakiwa na wananchi asishinde kwa sababu wananchi siyo wapira kura tena.

Ni sheria inayowapa watawala kuamua nani awe mbunge au diwani bila kujali kura. Ni sheria inayomtaka msimamizi wa uchaguzi kuamua kufuta majina ya wagombea. Ni sheria inayowapa nguvu tume ya uchaguzi kuteua wanayemtaka.

Ni sheria ambayo wakipiga watu kura let say 10 wasimamizi wanaweza kusema zimepigwa kura 1000

Kenya walitumia mfumo wa elektroniki kuhesabu na kutuma matokeo lakini Tanzania hata camera haitakiwi kituoni. Kwamba uchaguzi ni siri ya msimamizi na ukibaki kituoni wewe ni criminal

Kwa mapungufu haya ACT Wazalendo wanaweza kushinikiza uchaguzi kususia uchaguzi hadi sheria zibadilishwe?
 
..ACT Zanzibar hawataki kura ya mapema.

..Zanzibar kuna utaratibu wa kupiga kura siku mbili.

..siku ya kwanza ni kwa ajili ya vyombo vya ulinzi na wasimamizi wa uchaguzi.

..siku ya pili ni kwa ajili ya wananchi wote.

..ACT wanapinga utaratibu huo, na wameapa kuuzuia.
 
Back
Top Bottom