Je! Ada elekezi kutoka TCU litasaidia?

Je! Ada elekezi kutoka TCU litasaidia?

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2014
Posts
6,170
Reaction score
7,665
Tume ya vyuo vikuu imesema kuwa kuanzia mwaka wa masomo mwaka 2014/2015 nakuendelea, wametoa ada elekezi kwa kila chuo ili kupunguza ulipaji wa ada kubwa kwa vyuo binafsi na serikali.

ADA ELEKEZI Katika masuala ambayo yamekuwa tatizo kubwa kwa wanafunzi wengi na wengine hata kupelekea kushindwa kumaliza masomo yao ni suala la Ada na kumekuwa na utofauti mkubwa sana katika masuala ya ada kutoka chuo kimoja mpaka chuo kingine hususani katika vyuo vya watu binafsi au taasisi.

lakini kwa mujibu wa Afisa habari Mwandamizi toka TCU, Edward Mkaku amesema kuwa kwa mwaka huu wa masomo 2014-2015 Taasisi ya Vyuo Vikuu imekuja na mfumo elekeze wa ada kwa vyuo vyote na wanapaswa kuufuata,yaani kila chuo kimepangiwa Ada inayostahili kulipwa na wanafunzi kulingana na uwezo wa chuo husika na huduma itolewayo katika chuo husika.

Kitendo cha Tume ya Vyuo Vikuu kuja na mfumo elekeze wa Ada kwa vyuo vikuu itasaidia kushuka kwa Ada kwa baadhi ya vyuo vilivyokuwa vikichaji Ada kubwa kuliko huduma wanayoitoa.pia itasaidia hata wanafunzi kuweza kumudu Ada hizo katika vyuo hivyo. "Mkaku kuanzia mwaka huu kuna utaratibu wa Ada elekezi ambapo Tayari kila chuo kinapaswa kuufuata"

Je nini mtazamo wako katika hili... kweli ada inaweza kushuka lakini inaweza shuka kwa asilimia ngapi na itasaidiaaa au ndo zilee ahadi nying lakini utekelezaji hakuna.... jamani tujadili kwa pamoja tuone inakuwaje maana tcu wamesema hili lakini juzi kati tuu tumeona kilicho tokea UDOM je utaratibu ulikuwa bado haujawafikia toka tcu hawa wa UDOM au ilikuwaje... au tcu wana tupiga danganya toto

TOA MAONI YAKO ...
 
Inaweza kusaidia .mfano mwaka wa masomo 2014/2015 ada ya kcmc ilikua iongezeke lakin baada ya wanafunzi kufatilia kwa ukaribu TCU ada ilizuiliwa kupanda hivyo kubaki kama zaman
 
Sijui kama itafanikiwa kiutendaji, maana ugonjwa wa policy nzuri za maandishi lakini utendaji f bado ni sugu
 
mh.. siasa kila kona.. kama ni ya ukweli wametuokoa
 
Back
Top Bottom