Je, addiction ya sigara unaweza ukarithi?

flamini

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2015
Posts
533
Reaction score
586
Habari zenu wakuu?

Mimi ni kijana niliyekulia na kusoma katika mazingira ya dini na maadili,mimi toka nasoma najua sigara ni hatari kwa afya na matangazo na vitu nilivosoma kuhusu ubaya wa uvutaji sigara ni vingi kiasi kwamba nilijua mimi sitovuta kabisa sigara.

Toka naakili zangu nilikua namjua mjomba wangu ndo mvutaji sigara katika ukoo wetu mzima na nilikua sikai nae,baba yangu sikuwahi kumuona wala kusikia akivuta,bibiyangu mzaa baba ndo niliskia alikua anavuta zamani ila sikai nae wala sijawahi kumuona,kabla nilikua sina hata rafiki mmoja mvutaji.

Lakini mimi toka nipo form 5 boarding from nowhere nimejikuta nimeanza kua mvutaji kwa kujificha ficha mpaka leo nipo chuo tena nasoma mambo ya afya ndo wazee wanakuja kujua na baba yangu alikasirika sana na kunionya sana,yaani kakasirika kweli.

Kilichonifanya niandike uzi huu ni leo mida ya jioni wakati nimetoka nje kidogo na nyumbani kwetu nikajibanza sehemu na mshakiji mmoja jirani hapa nikwa nawasha sigara basi akaniambia hivi"wewe na baba yako wote mnavuta sigara ila hamjuani" aisee bado nusu moshi niumeze niliposikia hivo

Akaniambia mzee wako anavuta ila anajificha sana yaani sikuamini na ndo hapo nilipopata majibu ya maswali yangu ambayo nilikua najiuliza,nilikua najiuliza imekuaje mimi nimekua mvutaji sigara pamoja na mazingira yangu,kampani yangu pamoja na familia yangu kua hayaruhusu tena nimekua mvutaji kirahisi bila kishawishi chochote, Je hizi addiction unaweza ukarithi?Maana mi naona nimerithi.
 
Swali kwa wavutaji wa sigara.

Hivi kwanini mnapoenda haja kubwa huwa mnavuta sigara?

Haja kubwa na sigara vina uhusiano gani?

Tunaomba mfunguke na sie wengine tupate darsa kutoka kwenu
 
Sidhani kama unaweza kurithi, baba yangu alikuwa mvutaji sana wa sigara ila nashukuru aliacha! Mimi nilipofika umri ambao unatamani kujaribu kila kitu....nilivuta, lakini sikuipenda na ninaichukia sigara kuliko hata ninavyoichukia nyinyiem! Huwa nawashangaa wavutaji, kwa nini wanavuta kitu ambacho kwanza kina maonyo ya kuathiri afya! Acheni jamani kuvuta sigara!!
 
Swali kwa wavutaji wa sigara.

Hivi kwanini mnapoenda haja kubwa huwa mnavuta sigara?

Haja kubwa na sigara vina uhusiano gani?

Tunaomba mfunguke na sie wengine tupate darsa kutoka kwenu
inakufanya ujiskie haja ndo maana mtu anaenda chooni kuvuta haja ije,pia ni mazoea tu
 
yaani mkuu hiki kitu ni majanga,kuna ticha daktari tena ana masters lakini akimaliza pindi lazima utamkuta chemba anavuta sigara yaani ni aibu na hataki aulizwe chochote kuhusu hilo
 
mhhh kisayansi hauwezi kurithi ila hua naskia hivi vijitabia vinarithisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…