leekingroy
Member
- Jan 6, 2016
- 5
- 2
UTANGULIZI
Africa ni bara lenye Rasilimali za kutosha ambazo wazungu huzitumia kutokana na kwamba sisi watu wa Afrika tumeshindwa kuona umuhimu wake na mwishowe wanatengeneza bidhaa na kuzitumia wao na zikisha poteza thamani basi hurudisha Afrika na kutuuzia uchafu wao na kusema ni Imefanywa kuwa upya (refurbished) au imetumika (used) bado mpya.
Magari mengi sana (asilimia 99%) yanayo letwa Afrika kwa mauzo kama magari yaliyo tumika ni magari ambayo yamesha poteza kiwango cha kutumika tena katika nchi za wazungu walio endelea. Afrika kutokana na ufinyu wa teknolojia na kuwa na watu wengi ambao hawana ujuzi katika teknolojia na kushindwa kujiendeleza haswa katika kujitengenezea vifaa ndio inapelekea kwa urahisi kupokea magari ambayo talisha kwisha kiwango cha kutumika.
Imagine mtanzania anaringa barabarani kuwa ana gari jipya ambalo limesha kwisha ubora wa kutumika katika nchi ilipo toka kutokana na sheria za nchi hiyo kuweza kufanya vipimo na kuona kwamba muda wa gari hiyo umekwisha na halifai tena kutumika. Magari mengi sana Tanzania ni magari ambayo huletwa kuja kufia Tanzania na kutokana na kwamba yamesha poteza viwango, yakifika Afrika/ Tanzania yanakufa mapema kutokana na mafundi wetu pia kutokuwa na taaluma mahususi ya kurudisha ubora hata kwa kiasi fulani katika gari hizo.
Je, tutaendelea kupokea magari yenye viwango hafifu mpaka lini? Swali hili jipe jibu kwa kutafakari kwa kina, mpaka lini Afrika itakuwa ni dampo la kuuzia magari chakavu na yasiyo na viwango?
Gari hizo zinapofika nchini, lazima zifanyiwe tena check up au service kutokana na ukuu wake na kutojulikana muda mrefu kiasi gani zimekaa au kutumika namna gani huko zilipo toka. Bara la Afrika kutokana na umaskini wa wananchi, inapelekea wananchi wenyewe kutokuwa na elimu ya kutosha kujua thamani na ubora wa kuwa na gari jipya.
Afrika ya kusini ni moja ya nchi za Afrika ambayo imewekeza katika makampuni ya usafiri nankutengeneza magari yao wenyewe na kuuzia Afrika kwa gharama nafuu, lakini bado gharama ya gari ya Afrika kusini mpya ni kubwa tofauti na ile inayo toka nje ya bara la Afrika. Hapo tunagundua kuwa licha ya hali duni ya wengi wa Waafrika, pia hata elimu nayo inachangaia kusababisha hali ya umaskini wa taaluma katika kufanya maamuzi katika mambo yanayo leta maendeleo.
Watanzania wengi hununua magari yaliyo tumika ambayo hayana tena viwango vya kutumika nchi yalipo tokea, magari hayo hufika Tanzania na kutokana na mafundi wetu ni mafundi wa mitaani ambao hawana taaluma halisi, huyarekebisha kwa kiwango kidogo sana na yanapo haribika, huachwa yakioza na kuharibu mazingira.
Magari mengi yanayo kuja afrika yaliyo tumika huwa ni magari ambayo licha ya kuwa hayana thamani na viwango kutumika nchi yalipo toka, pia hata teknolojia yake huwa imepitwa na wakati na kupelekea kuwa hayafai tena barabarani. Nchi nyingi sana zimehamia katika magari yenye teknolojia mpya na yenye kutambua mazingira kwa ajili ya kiusalama na urahisi wa kusafiri na pia yana teknolojia ya kupunguza uwezekano wa ajali kutokea. Magari mengi yaliyo Afrika hayana teknolojia hiyo, ndio maana ajali haziwezi epukika, magari kama Tesla yanatumia umeme wa betri za lithium ambapo hazitumii engine ya mafuta bali hutumia mota na magari hayo huchajiwa kama simu na kutumika bila kuharibu mazingira, kwa nchi kama Tanzania mwananchi akinunua IST anajisifu kuwa na gari la kisasa ingawa gari hilo ni la miaka 10 na zaidi (umri wa kiajana wa darasa la 4).
Je? Ni sawa kuendelea kuingiza magari ya namna hiyo? Elimu itolewe, tuache kuagiza magari yaliyo pitwa ma wakati na tuwe na magari yanayo kwenda na wakati, pia itasaidia haswa katika kutunza mazingira.
Picha chanzo: CarWow - AMG MB | Japanese Used Cars - Fuso Truck | Jaguar UK - Land/Range Rover | Camera - Toyota Voltz.

Upvote
2