Je, Ajira sio Agenda tena?

Je, Ajira sio Agenda tena?

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
15,460
Reaction score
24,233
Hapa nataka kuwauliza watunga Sera na Vyama vya Siasa..., ila kabla ya yote kwanza ninanukuu Babu wa Chama Tawala cha Sasa kilivyosema na kilivyokuwa kinaamini.... (Extract kutoka Hotuba ya Mwalimu Nyerere)
  • CHAMA CHETU KINASEMA - mtu mwenye Afya ambaye tumeshindwa kumpa njia halali ya kujipatia riziki yake. Nawaomba ardhi - hakuna ardhi; hamnipi ardhi, Mnasema "Ardhi hakuna". Naomba kazi ya kibarua basi, Nipeni basi ya kibarua, "Hamnipi kazi ya kibarua. Mimi niko tayari kabisa kufanya kazi au ya kulima au ya kibarua chochote nipeni. Hamnipi Chama Chetu kinasema MTANILISHA.

Sasa kuna Kasumba imetokea ya hawa walioshiba kuwaambia vijana wetu kwamba mkajiajiri yaani eti wafundishwe kujiajiri eti vijana hawa ni wavivu na wanashinda vijiweni..., Sasa kwa sisi tuliokula chumvi tukikumbuka kuna kipindi tulikuwa tunachagua kazi (ualimu, upolisi, na kada nyingine watu hawaendi) leo hii tangaza kazi yoyote utapata watu mara 1000 ya wahitaji (kwahio utaona kwamba uhitaji ni mkubwa), na tuliowapa kazi ya kutuwekea mambo sawa hawajayaweka sawa (kwanza ndio yanazidi kwenda kombo)

Na hawa madogo sio wavivu kabisa (kuna wasanii wamejiajiri ndio wanatupa burudani) wengine hadi wameingia kwenye sekta za udangaji, mitaani wachuuzi kibao, watu wanaenda kulima masoko hakuna watu wapo desperate ndio maana wengi wanadumbukia kwenye kamari na mitego ya investment za kitapeli.., Tatizo ni kwamba hakuna misingi (infrastructure) bora ya kutumia nguvu kazi hii...

Sasa wanaosema watu wajiajiri how? Wakaongeze idadi ya wachuuzi na madalali ? Yaani tumesomesha watu kwa kodi zetu ili waje watuuzie bidhaa za mchina ?.., Na zile kazi hot cake ambazo tunaweza kutumia automation tunawapa watu wa mbali waje wafanye ili sisi tuendelee kuwa wachuuzi !!!!

Tunahitaji kurudisha fikra zetu nyuma.., as what's going on is not working and it will get worse......
 
KUNA SHDA SANA KWNYE MFUMO WA ELIMU HI.WENZETU NIGERIA WAMEJIKWAMUA KTK HILI WALIKUWA KM SISI.
 
KUNA SHDA SANA KWNYE MFUMO WA ELIMU HI.WENZETU NIGERIA WAMEJIKWAMUA KTK HILI WALIKUWA KM SISI.
Best Modal wala sio kuwa kama Nigeria..., Kwa nchi yenye mbuga kama hii na Mambo mengi ya Kitalii mfano niliweka hapa huu uzi


Haipaswi tuwaambie watu eti tunawafundisha wakajiajiri (mtaa unahitaji discipline na experience na mtaa sio wa kila mtu ni wa wachache) inabidi kuwepo na miundombinu ya kuweza kuwabeba wengi ambao wao wanaishi mshahara kwa mshahara mwisho wa siku wapate pensheni wasubiri vifo...

Hili la kumwambia kila mtu aingie kitaa wakati hao wanaosema / watoa kauli wenyewe hawaingii kitaa ni kuuziana mbuzi kwenye gunia....

Na wanasiasa tena hii sio agenda tena ya kuleta ajira yaani hilo walishamalizana nalo sasa sijui cha maana zaidi ya ujira kwa watu ni kitu gani....
 
Back
Top Bottom