Je Alicho Fanya Eric Omondi Ni sahihi?

Je Alicho Fanya Eric Omondi Ni sahihi?

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2014
Posts
6,170
Reaction score
7,665
HABARINI! TOKA jana kwenye mitandao ya kijamii Mchekeshaji Erick Omond amejiwa juu na baadhi ya watu kwa kile Alicho Fanya na kuleta mvutano mkubwa sana katika Imani!

Mimi ni mkristo,Lakini sijaona Kosa kwa kile Alichokifanya Erick Omondi! kabla ya Kuja kumuhukumu Erick Omond .....Tujiulize Je Erick Omond ni nani na anafanya nini? ERICK ni Mchekeshaji na anafikisha ujumbe kwa njia ya kuchekesha na kuimba!

Sasa kile alichokifanya ni moja ya uigizaji wake na Lengo lake ni kufikisha ujumbe! Jumbe ulifika tatizo liko wapi? Tujiulize Je mtu akiigiza kama Rais ni kweli anakuwa Rais? au mtu akiigiza Ana maambukizi je kweli anakuwa mayo?

Moja ya watu walio Kuja juu ni baraka De prince Lakini mm sioni kama ni sawa kumuhukumu Eric kwa Alicho fanya
1480771425963.png


Sasa Tujiulize wote Je Alicho Fanya Eric ni Sahihi? Kwangu mimi yupo sahihi
 
Tofautisheni kejeli na kuigiza, huyo amekejeli dini ya watu, sema wa kristo huwa tunakuwaga na mazoea ya ajab ajab kwenye dini yetu, wakati wenzetu waislam jaribu hata kuwa tania kidogo kuhusu dini yao uone, na kwa hilo nawapongeza, we must respect our entity tuache jokes na Yesu Kristo hebu tujifunze kwa wenzetu kuheshim tunacho kiamini.
Omondi alikosea sana
 
Tofautisheni kejeli na kuigiza, huyo amekejeli dini ya watu, sema wa kristo huwa tunakuwaga na mazoea ya ajab ajab kwenye dini yetu, wakati wenzetu waislam jaribu hata kuwa tania kidogo kuhusu dini yao uone, na kwa hilo nawapongeza, we must respect our entity tuache jokes na Yesu Kristo hebu tujifunze kwa wenzetu kuheshim tunacho kiamini.
Omondi alikosea sana
Yale maneno yaliyowekwa juu ya msalaba yanadhihaki. Sio mazuri kabisa
 
Yale maneno yaliyowekwa juu ya msalaba yanadhihaki. Sio mazuri kabisa
Ndugu, umesahau kuwa Yesu alisulubiwa pamoja na watu wawili.. Yule wa mkono wa kuume ndio huyo Omondi amemuigiza..

Pitieni vizuri biblia zenu kabla ya kumlaumu Omondi..

Dhana ya kusulubiwa haikuwa kwa yesu pekee..

Omondi amemaanisha yule mwizi wa mkono wa kuume wa Yesu aliyenena maneno ya hekima kwa yesu na akasamehewa kabla yesu hajakata roho..
 
Mungu wetu anajipigania mwenyewe, huyu jamaa asipoomba toba kwa kitendo hiki, yatakayomsibu asilie na mtu.
Wengi hamkumuelewa Omondi..

Omondi amemuigiza yule mwizi wa mkono wa kuume wa yesu pale msalabani..

Yesu alisulubiwa katikati ya watu wawili..
 
Yesu Kristo wa Nazareth hakua wa kwanza kusulubishwa msalabani, walihukumiwa hivyo wengine kabla yake, na Hata siku anasulubiwa kulikua na wengine wawili nao waliangikwa msalabani.

Ikumbukwe neno linatukumbusha kuacha dhambi na kujitenga na uovu. Kuendelea kutenda dhambi ni kumsulubisha Kristo kwa mara ya pili Hata kama haufurahishwi na hili tukio la igizo la kutundikwa msalabani.
 
Back
Top Bottom