Je, anasumbuliwa na nini?

Desire Dizaya

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2015
Posts
6,476
Reaction score
11,659
1.anahisi mwili wa baridi sana lwa ndani hadi anaumia..anakosa nguvu mwili unalegea.
hali anayojiskua analia kama mtoto mdogo

2.anahisi hofu ya kufakufa mda wote.analia.usiku anaogopa hata kufumba macho anahis atakufa kabisa

3.akiona kitu chenye damu mfano nyama ya ng'ombe mbichi.hata kama imepikwa au ikiwa karibu yake tu nae anatokwa na damu kama vile akiwa period.lakini hii damu inatoka kwa wingi kuliko kawaida..na hata ukiweka nguo inalowa chapachapa..akila ndo kabisa inaflow zaidi ya wiki mbili

3.anahisi kuna kitu kwenye tumbo lake..kuna siku alikua anaharisha vitu vyeusi kama grease
thn akawa anataka kutapika anahis kitu kinataka kutoka tumboni lakini wapi.anajikamua hakitoki.


wenzangu bado ndugu yangu anaumwa..kama kuna aliewahi kupata matatizo kama haya anisaidie solution.
ameemda muhimbili,agakhan,hindu mandal,burhan,jakaya kikwete cardiac inst na kwingineko

kapimwa kila aina ya vipimo
MRI,ct scan..xrays
kapimwa ubongo,figo,kibofu,tumbo,kizazi,kifua,Macho,mapafu,koo,damu.mwanasaikolojia etc
hakuna kitu..hawaoni tatizo lolote

tumeenda makanisa kibao ya kila aina..
miti shamba nayo hakuna matokeo
sheikh mmoja hakuna matokeo
tumetumia pesa nyingi sana..mamilion yameenda

tunahis ni mambo ya kishirikina..basi hata anaemjua wa kutatua hili tatuzo alie karibu na dar anisaidie..
 
Ninaomba nikushauri jambo moja kubwa.
Kwanza ni nyie na mgonjwa kuhusu imani zenu.Kama imani ipo nusu kwa hospitali hata mngepiga xray,MRI ngapi hapatakuwa na mafanikio.Hii ni kwa sababu ni uvumilivu mkubwa unaohitajika katika hospitali kubwa.Kwa mfano MRI itafanyika na radiologist ataisoma na kutoa ushauri wake.Baada ya hapo inatakiwa urudi kwa daktari na mara nyingi madaktari wa ngazi hii hawapatikani ki urahisi,panahitajika uvumilivu mkubwa (kasafiri,njoo wiki ijayo,anaumwa n.k).Bila kuwa na uvumilivu utakimbia.
Rudini hospitali mkiwa na nia moja na tatizo hili litamalizika na hamtaendelea kupoteza pesa kwa matapeli!!!
 
asante..
sijui kama umefikiria kwakina matatizo nloorodhesha lakini?
 
asante..
sijui kama umefikiria kwakina matatizo nloorodhesha lakini?
Nimefikiria kwa kina mno na nina miaka 33 ya kutibia binadamu na pia ni mtaalamu wa medical anthropology.
Hivyo ninaamini ninachozungumza.
kwa mwendo wa kuombewa,kanisani,Shehe na waganga wa kienyeji nimeshakusoma vizuri.
Nakukumbusha tu,vipi kuhusu mtoto aliyekuwa anaishi kwa kunywa mafuta ya kula shida iliishia wapi?
aamua moja,ni hospitali na kama ni kufa ndugu yangu afie hospitali"Utaona matokeo.
 
Huyu mgongwa anaendeleaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…