Je, asili ya Washirazi ni Persia?

Je, asili ya Washirazi ni Persia?

Abunwasi

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2009
Posts
5,486
Reaction score
3,473
Zanzibar kuna wenyeji wengi hasa Kaskazini Unguja, Tanga, angani, Mombasa nk. hujinasibu kuwa wao ni washirazi.Kuna wakati kule mombasa walikuwa wanaitwa wageni na wengi ilibidi wajichanganye hivyo wengine wakajiita wadigo ili mradi waweze kuishi kwa amani.

Kwa Zanzibar Umuhimu wao unajionyesha hata kwenye siasa kwani ninasikia walikuwa na chama kiitwacho Shirazi Party ambacho baadaye kiliungana na Afro na kuitiwa Afro Shirazi Party na mwishowe kuwa sehemu ya mapinduzi ya zanzibar.

Hawa ni watu walitokea wapi? na asili yao hasa ni ipi? Ningependa wana historia wachangie kwenye hili ili lieleweke vizuri.

Katika kudadisi kwangu kwanza washirazi hawapendi kujinasibu na waarabu na ndiyo maana ilikuwa rahisi kwao kushirikiana na African Association kuliko Hizbu.

Nilichokipata mimi[na ambacho ningependa wajuzi zaidi wachangie] ni kwamba asili ya washirazi ni Persia ya zamani na inasemekana kuwa katika kile kipindi cha utata wa ukhalifa baada ya kufariki Mtume Muhammad (SAW), ambapo baadhi waumini waligawanyika wakati wengine walitaka sayyed na Ally apewe nafasi hiyo na wengine wakataka waraka wa mtume ufuatwe. Hali hiii ilileta farka na ilienea hadi persia ambapo sayyed na ally alikubalika sana[Jee hiki ndicho chanzo cha Shi?[wajuzi tusaidieni].

Kule h persia kwa wale wachache ambao walitaka utashi wa mtume utumike katika uchaguzi wa ukalifa wakawa persecuted na kulazimika baadhi kukimbia. Wengine walikuja huku pwani ya afrika ya mashariki. Hawa jamaa hawakuwa traders bali walikuwa craftsmen wakitengeneza milango, viti majahazi na walipokuja huku hiyo ilikuwa kazi yao kubwa na hivyo kuthaminiwa sana na falme za Pwani ambapo walihusika sana na shughuli hiyo[Milango ya Zanzibar, Madirisha]ingawa wengine wakaingia katika uvuvi na biashara.

Ingefaa sana kama wajuvi wa historia wangeongeza nyama kwenye historia ya kundi hili historia ya jamii hii ya kizanzibari likae sawa
na vile vizazi vya sasa na vijavyo vifahamu asili yao.

NAWASILISHA
 
Back
Top Bottom