Je, Azam wamedhamiria kuchukua nafasi ya Simba Klabu Bingwa au wanatuzuga tu?

Je, Azam wamedhamiria kuchukua nafasi ya Simba Klabu Bingwa au wanatuzuga tu?

Smt016

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2016
Posts
3,012
Reaction score
4,300
Ukiangalia namna viongozi wa Azam na wachezaji wake wana hali ya usimba na uyanga mle. Kitendo cha Azam kufungwa goli tatu na Simba kulileta tafsiri ya aina yake kwasababu Azam walihitahi tu point moja kwa Simba ili kujiwekea uhakika wa kucheza klabu bingwa ila cha ajabu tuliona jinsi Azam walivyofungwa.

Mechi mbili za Azam zilizofuata ni kama watu wameanza kuona kama vile Azam wameamua kuwa serious ila binafsi bado sijawa na hiyo imani hadi nione mechi ya mwisho ya Azam dhidi ya Geita.

Hadi sasa nafasi ya pili ipo mikononi mwa Azam kwavile anahitaji ushindi wa aina yoyote ule, wakati Simba wao wanahitaji ushindi wa goli nane dhidi ya JKT. Ni jambo ambalo linawezekana kwa match fixing pekee. Jevni kweli Azam wameamua kutoka kwenye siasa za Simba na Yanga?

Je, wanamaanisha kweli kuutaka nafasi ya pili au ni zuga tu mwishoni wataachia?
 
Ngoma nzito, wachezaji wengi na uongozi wa Azam wanataka Simba ichukue nafasi ( refer 3 -0 za mchongo ), TFF wanataka simba ichukue nafasi ili kupata sifa , ila Feitoto binafsi anataka kufunga magoli mengi achukue golden boot, benchi la ufundi la Azam linataka timu ichukue nafasi ya pili iliyo mkononi ili kujaza CV yao kwa kucheza CAF champions league.

Tusubiri mechi ya mwisho itajulikana. Azam wakijiangusha mechi na Geita tutaona na nitamwambia mwanangu shabiki wa Azam ahamie Yanga na jezi za Azam sitamnunulia tena shabiki wao kindakindaki my 8 years boy.

Hii nafasi ya pili Azam wakiwapa Simba watapoteza mashabiki wengi sana na kushusha thamani ya timu yao.

Azam mbele kwa mbele!! Onesheni uwezo wenu msijishushe. Huu ni wakati wenu kwenda Africa msifanye ujinga, Simba ni jumba bovu liacheni lianguke!!
 
Huyo dogo ukiona uvivu kumnunulia jersey ya Azam nipe mm hio kazi niwe namnunulia hahahah (jk)

Ila mkuu, Azam lazima abebe nafasi ya pili msimu huu, kwa udi na uvumba
 
Nafikiri Azam wana nafasi ya kuvuna mashabiki wengi kutoka simba kama wakifanya vizuri
 
Ni bora Simba imalize ya 3 na kujipanga upya. Bado haina timu ya kushindana champions league na inahitaji kusajili wachezaji kama 8 wapya na kutengeneza uongozi unaosikilizana na timu yenye ari mpya.

Wapunguze pressure msimu ujao huku wakitafuta zaidi kikombe cha ligi ili kurudisha imani kwa wanachama na mashabiki wake.

Wakubali kushiriki shirikisho ambapo hakuna pressure.

Huo ni ushauri wangu kama shabiki wa Coastal Union.
 
Mpira unadunda tutaona itakavyokuwa,
What if geita akamgonga azam, bado itakuwa match fixing? au geita kwa namna yoyote hapaswi kumfunga azam
 
Mpira unadunda tutaona itakavyokuwa,
What if geita akamgonga azam, bado itakuwa match fixing? au geita kwa namna yoyote hapaswi kumfunga azam
Umeelewa niliposema neno kutuzuga? Maanake hata Azam wanaweza kuamua kuwaachia Simba waende kwa kucheza chini ya kiwango ili kutoa sare au kufungwa. Soma vizuri mada
 
Mpira unadunda tutaona itakavyokuwa,
What if geita akamgonga azam, bado itakuwa match fixing? au geita kwa namna yoyote hapaswi kumfunga azam
Ndio maana nikauliza maswali mengi kwasababu hatima ya Simba ipo kwa Azam fc
 
Ndio maana nikauliza maswali mengi kwasababu hatima ya Simba ipo kwa Azam fc
Nimekusoma na nimekuelewa,hapo kwenye kutuzuga tutajuaje kama ametuzuga ndiyo maana nimehoji tu,kwamba geita hapaswi kumfunga azam hata apate chance,kwa mtazamo wako nimeona kwamba unaamini azam ndiyo pekee ataamua simba awe wapi..
 
Wadau wengi wa michezo tunatamani kuona mshindi wa pili anapatikana kwa haki, na siyo kwa magumashi.
 
Back
Top Bottom