Je Bayer 04 Leverkusen kubeba ubingwa wa Bundesliga Leo?

Je Bayer 04 Leverkusen kubeba ubingwa wa Bundesliga Leo?

Goguryeo

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2019
Posts
3,003
Reaction score
5,653
Bayer 04 Leverkusen leo ipo uwanjani kukipiga na werder Bremen majira ya saa 06:30 pm (12 na nusu jioni).

Ikumbukwe kwamba Bayer Leverkusen wanaongoza ligi ya Bundesliga wakiwa na point 76 huku wakiwa wamecheza michezo 28 na huu wa Leo utakua wa 29.

Nafasi ya pili wapo Bayern Munich wakiwa na michezo 29 kibindoni na pointing zao 63. Hivyo basi gape lao la point ni point 13.
Screenshot_20240414-174652 (1).png


Iwapo Leo Bayer Leverkusen atashinda mchezo wao ,watafikisha pointi 79 ambazo hazifikiwi na timu ya pili/yoyote hata wakishinda michezo yao yote iliyobaki.

Hii itakua ni mara ya kwanza kwa historia ya club yao kutwaa taji la Bundesliga huku wakiwa na michezo mitano (5) mkononi kuelekea mwisho wa ligi hiyo kwa msimu huu ambayo inajumuisha timu 18 yenye jumla ya michezo 34 kwa msimu.

Mara ya mwisho kukamata nafasi za juu ilikua ni msimu wa mwaka 2010/2011 ambapo Bayer Leverkusen walishika nafasi ya pili kwenye Bundesliga na wamefikia hatua hiyo mara 5 kihistoria.

ni P.schick
au V. Boniface
au G.xhaka
au J.hoffman nk
au Xabi Alonso
images (1).jpeg

Je nani kuibeba Bayer Leverkusen leo ?

Je Bayer Leverkusen watatwaa ubingwa wa Bundesliga Leo na kuweka historia ?

Em tusubiri tuone ........
20240414_175942.jpg
20240414_180004.jpg

20240414_175947.jpg

20240414_175952.jpg


20240414_181928.jpg

20240414_204708.jpg

20240414_204629.jpg
 

Attachments

  • 20240414_204629.jpg
    20240414_204629.jpg
    1.4 MB · Views: 3
  • 20240414_204629.jpg
    20240414_204629.jpg
    1.4 MB · Views: 3
Wamejitafuta sana wahuni bayer 04

Huwa nawakumbuka kwa fainali ile ya uefa dhidi ya real madrid zidane akifunga goal tamu kwa guu la kushoto

Nusu fainali bayer walicheza na manchester united game zote zikiisha kwa sare za magoli wakaenda fainali kwa goal la ugenini
Michelle ballack akiwa wa moto katikati ya dimba
...
They deserve to win bandasliga kwani washataniwa sana kuwa ni cursed team hatimae wamejitafuta
 
Back
Top Bottom