CalvinKimaro
JF-Expert Member
- Sep 11, 2017
- 245
- 314
Siku mbili tatu hizo zilizopita mtaalamu wa UN kuhusu haki za binadamu alitoa taarifa yake baada ya kumtembelea JULIAN ASSANGE. Ni mmiliki wa WikiLeaks ambaye kwa sasa anashikiliwa na Serikali ya Uingereza akisubiri uamuzi wa ama kumkabidhi kwa serikali ya Marekani au la. Alikamatwa mwezi April baada ya kujificha ndani ya ubalozi wa Ecuador mjini London kwa takribani miaka 7.
Mtaalamu wa UN anasema mazingira aliyowekwa Assange ni hatarishi mno na wakati wowote yanaweza kusitisha uhai wake. Anadai Assange anateswa! Anahitimisha Kwa kusema ikiwa Serikali ya Uingereza haitazingatia haki zake kama mwanadamu Assange anaweza kufa wakati wowote ule.
Sasa kina AI na HRW ndio wametoa taarifa zao juzi lakini hawakugusia suala la Assange. Wao wanamuona Kabendera Tu, Amnesty International makao makuu yako London ambako ndiko anakoteswa Assange, BBC Tumbili (aka Swahili) Service iko London. Hayathubutu kumtaja Assange.
Tumbili wetu walio BBC wao kazi kudai kina Azori ambao hakuna ushahidi wowote dhidi ya Serikali ya JMT. Huyu Assange ambaye wanajua yuko mikononi mwa serikali iliyo London hawana habari. Tumbili Service badilikeni. Thubutuni kumtetea Assange tuone kama hamkufurushwa mrudi kwenu!