Masokotz
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,713
- 6,121
Katika siasa za nchi yetu sasa ina makundi matatu
Kundi la kwanza ni la Watangazania,Wapinzania na Wagombania.
Watangazania Wamejaa sana CCM hasa baada ya Mwenyekiti kusema kwamba ukikosa ubunge unaweza pata UDC na Hata ukapata Ukurugenzi.Wagombania wako busy kwenye majimbo wanasuka mikakati kuhakikisha kwamba wanapata nafasi za kuingia mjengoni na Wapinzania wako nao wanansuka mkakati kuhakikisha kwamba nao wanashika Dola na kuwang'oa CCM madarakani.
Mkakati wa Wapinzania sasa umewiva,Wameamua kufanya jambo ambalo hakuna anayelitarajia nalo ni kumsimamisha Bernard Membe kama Rais, na Kisha Tundu Lissu kama Mgombea Mwenza.
Membe anawakilisha uasi ndani ya CCM na ataungwa mkono na magwiji wote ambao JPM amepania kuwakata katika kura za maoni za Ubunge wakiwamo kina Nape Nnauye,Yusuphu Makamba,na wengine wengi ambao ni wapinzania wa ndani ya CCM ambao JPM amepania kweli kuhakikisha hawarudi bungeni kwa sababu ya tofauti zao kiitikadi ni kimsimamo.Hivyo basi atakaposimama Membe hawa wote wataungana naye kuhakikisha JPM anatoka ikulu liwake jua inyeshe mvua.
Tundu Lissu anawakilisha wana Mageuzi,wanaonyonywa,waliobinywa,waliodhulumiwa.Anawakilisha watu waliopotezwa kama kina Ben Saanane,Azory na wengine wengi.Anawakilisha wanaoishi kwa hofu ya kupoteza uhuru wao.Anawakilisha waliofungwa gerezani kwa kesi za kubambikiwa,Anawakilishwa waliopteza ajira,walipoteza uhuru,Wanaodhulumiwa na wateule wa JPM.
Kinachosubiriiwa kwa sasa ni nafasi ya Zitto Kabwe na ACT ili hatimaye msimamo upinzani uwe thabiti.
Kwa mpangilio huu kwa hakika CCM haitaweza kushinda ndani ya sanduku la kura wala nje ya sanduku la kura,Sio jeshi wala policcm watakaoweza kuiba kura za wananchi ambao watakuwa wamepewa kile wanachotaka.
Mkakati huu rahisi nimeujadili na watu wengi na kwa hakika ni mkakati thabiti kabisa ambao unaenda kuleta ushindi kwa asilimia kubwa.
Niwatakie kila la heri katika kuleta maendeleo ya nchi na kujenga TAIFA.