Je biashara gani ambayo Mwajiriwa anaweza kufanya ili kuongeza kipato?

jb87

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2012
Posts
250
Reaction score
445
Habari zenu waungwana!

Mimi ni mwajiriwa wa serikali, lakini kwa kipindi kirefu sana nimekuwa nikitamani kujihusisha na biashara walau kukuza kipato cha familia.

Bahati mbaya sijawahi kujaribu biashara yoyote, sijui ni uwoga wa maneno ya watu maana mara nyingi nimekuwa nikisikia watu wakilalamika kuwa biashara zao zimeanguka sababu wanakosa muda wa kuzisimamia.

Naomba mwenye uzoefu, je kwa mtumishi/mwajiriwa ni biashara gani ambayo unaweza kuifanya with the little supervision time you have na isikuangushe.

Naomba ushauri wa kujenga waungwana sio kejeli, mi naishi mkoa wa kilimanjaro. karibuni wenye uzoefu tafadhali natumai ushauri wenu utasaidia wengi.

Nawasilisha
 
Ukitaka biashara isiyokuumiza kichwa
1. Fanya biashara ya kitu unachokipenda na unakijua, preferably kulingana na elimu yako.

2. Kama uwezi kusimamia mwenyewe, msimamizi/wafanyakazi sahihi ndo kila kitu. Ukibugi hapo tu umefeli.

3. Usiwe mvivu kusoma, yaani akikisha kila siku unapata walau dakika kadhaa za research.

Watu wakijua serikalini unafanya nini, nadhani itakuwa rahisi ku suggest biashara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fanya BIASHARA ya Duka tu Mkuu...!

Hii ni Biashara Mama/Baba maana karibu kila mmoja ameweza KUIMUDU.

Muda na Faida yako ni pale tu unapoamua KUJITOA/KUJITOLEA kuumia.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…