John Magongwe
Member
- Jan 4, 2024
- 71
- 119
Je, Binadamu Anaweza Kuwa Mtakatifu
Utakatifu ni Nini
Utakatifu ni ile hali ya kuwa safi mbele za Mungu, kumhofu yeye na kumuogopa yeye na kujitenga mbali na dhambi. Neno “Mtakatifu” lina maana mbili katika moja; Yaani kutengwa na dhambi kabisa na pili kuwekwa wakfu/ maalum kwa ajili ya kazi/matumizi ya Bwana. Hivyo, Utakatifu ni kutengwa na kujitenga na dhambi.
Tumeitiwa utakatifu, na lazima tuwe watakatifu katika mwenendo wote: mbele za watu na tukiwa peke yetu sirini.
ZIPO AINA TATU ZA UTAKATIFU. Aina hizo ni utakatifu wa mwilini, utakatifu wa rohoni na utakatifu wa mwilini na rohoni.
Utakatifu wa Mwilini
Ni ile hali ya kuuweka mwili katika viwango vya kumpendeza Mungu, ikiwemo kuvaa vizuri kiasi kwamba mtu akikutazama, anaona ushuhuda wa Kristo katika uvaaji wako na muonekano wako. Kwa ujumla, mtu anaona unadhifu katika muonekano wako.
Vile vile utakatifu wa mwilini unahusisha, kujilinda na matendo yote ya mwili yanayotajwa katika Wagalatia 5:19-20, yakiwemo uasherati, ulevi, kujichua, kujichubua na mengineyo. Ni kujilinda pia na uvaaji wa vitu kama vile hereni, mikufu, bangili, rangi usoni, mtindo wa nywele bandia na uvaaji mwingine usio na ushuhuda.
Mtu anaweza kuwa na utakatifu huu wa mwilini, lakini ule wa rohoni akaukosa. Anaweza kuwa na muonekano mzuri sana wenye ushuhuda, lakini akaukosa ule wa rohoni.
Utakatifu wa Rohoni
Utakatifu wa rohoni ni ule unaohusisha, matendo yote ya rohoni yanayompendeza Mungu.
Hii ni pamoja na kuomba, kutoa sadaka (Mathayo 6:4), kumwabudu Mungu katika roho, kujifunza na kutafakari Neno la Mungu. Vile vile unahusu upendo, uvumilivu, utu wema, na kiasi.
Wagalatia 5:22 “Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, 23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria”.
Ni rahisi sana mtu kuwa mtakatifu mwilini na asiwe mtakatifu rohoni, lakini si rahisi kukuta mtu mtakatifu rohoni na mwilini akawa si mtakatifu.
Utakatifu wa Mwilini na Rohoni
Utakatifu wa mwilini na rohoni ni ile hali ambapo mtu anakuwa na ushuhuda wa ndani roho yake na nje ya mwili wake. Na huu ndio utakatifu Mungu anaouhitaji kwetu.
1 Wakorintho 7:34 “Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana, apate kuwa mtakatifu mwili na roho”.
Utakatifu wa mwilini na rohoni ndio msingi wa sisi kumwona Mungu sawasawa na ile Waebrania 12:14: “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao”.
2 Wakorintho 7:1 “Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu”.
Viwango vya Utakatifu
Katika kuwa watakatifu wa mwilini na rohoni ni lazima viwango vyetu viwe juu zaidi ya watu wasio wa Kristo.
Mathayo 5:20 “Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni”.
Maana yake ni kwamba kama kumcha Mungu basi ni lazima tuwazidi wa imani nyingine, kama kuvaa kwa staha ni lazima tuwazidi watu wengine wote wasio wa imani, n.k.
TUNAPATAJE UTAKATIFU
Kuzishinda Tamaa Zetu
Dhambi yoyote kabla haijaleta madhara huwa inaanza kama mbegu ndogo. Biblia inasema chanzo cha dhambi ni tamaa.
Yakobo 1:14 “Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa. 15 Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti”.
Unapokuwa na uwezo wa kuzitawala tamaa zako, basi dhambi kwako itakuwa mbali, na hivyo siku zote utajiweka katika hali ya utakatifu.
Kukaa Mbali na Vichocheo Vyote vya Dhambi
Dhambi inayo vichocheo, kama vile hasira ilivyo na vichocheo. Kwa mfano vichocheo vya dhambi ya uasherati ni utazamaji wa pornography, mazungumzo mabaya na ya mizaha, makundi mabaya ya watu, uvaaji mbaya, filamu za kidunia ambazo asilimia kubwa maudhui zake ni kuchochea tamaa ya zinaa, vile vile magroup na kurasa mbalimbali katika mitandao ya kija mii kama vile facebook, whatsapp, instagram na mengineyo.
Kuomba na Kujifunza Neno la Mungu
Tunapokuwa waombaji, katika ulimwengu wa roho shetani na mapepo yake yananakaa mbali nasi. Hivyo na viwango vyetu vya utakatifu vinapanda. Vile vile, tunapokuwa watu wa kujifunza Neno la Mungu, tunakuwa tunatakasika kwa sababu Neno la Mungu lina maonyo ndani yake, na linatufunza na kutukumbusha kudumu katika imani na utakatifu.
Kuwa mtakatifu kunamaanisha kuishi maisha yetu kwa njia inayoangazia utukufu wa Mungu, badala ya kufuata njia za ulimwengu (Warumi 12:1-2). Inamaanisha kuwa tunahitaji kutii sheria ambazo Mungu aliweka kwa ajili yetu katika Biblia. Inachukua nidhamu kufanya hivi, na siyo rahisi kila wakati.
Kwa hiyo, kwa binadamu, utakatifu ni ile hali ya kuwa safi mbele za Mungu, kumhofu yeye na kujitenga mbali na dhambi. Binadamu anaweza kuwa na utakatifu wa mwilini, utakatifu wa rohoni, na utakatifu wa mwilini na rohoni. Binadamu anapata utakatifu kwa kuzishinda tamaa zetu, kukaa mbali na vichocheo vyote vya dhambi, na kuomba na kujifunza Neno la Mungu.