Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Hii ni Makala yangu kwenye gazeti la Nipashe.
Wiki mbili zilizopita kwenye safu hii niliandika mada ya kumpongeza Spika wa Bunge, Dr. Tulia, kwa kazi nzuri aliyoifanya kwenye Mabunge ya Dunia, IPU kwa kuwakoromea maspika wenzake wa nchi za mabeberu, kuziburuza nchi za Afrika. Nikamuomba Spika Dr. Tulia, atumie tone ile ile katika kuliendesha Bunge letu litimize majukumu yake kikamilifu ikiwemo kutunga sheria na kuisimamia serikali kikamiifu. Pongezi Spika Dr. Tulia, Umeonyesha Uwezo, na Unaweza!, Jee tumshauri Dada Mkubwa, ikimpendeza, ampishe tuu Dada Mdogo Kwenye Lile Jambo Letu Lile? tena sikuishia hapa, nikamshauri hata Dada Mkubwa kumpisha Dada Mdogo kwenye lile jambo letu Pongezi Spika Dr. Tulia, Umeonyesha Uwezo, na Unaweza!, Jee tumshauri Dada Mkubwa, ikimpendeza, ampishe tuu Dada Mdogo Kwenye Lile Jambo Letu Lile?
Makala ya leo, naligeukia Bunge, Bunge ndicho chombo kikuu cha uwakilishi wa wananchi, Bunge likisema ni wananchi wamesema, na kazi kuu ya Bunge ni kutunga sheria na kuisimamamia serikali, makala ya leo ni maswali kuhusu Mhimili wa Bunge na Mhimili wa Mahakama. Je Bunge letu ni linatunga kweli sheria, au linapitisha miswada ya sheria inayotungwa na Serikali?. Kwanini Mhimili wa Mahakama, unaliogopa hivi Bunge?.
Msingi wa maswali haya ni muendelezo wa kuwaelimisha Watanzania kuhusu katiba, sheria na haki, kwa dhima ya mtunga katiba alidhamiria nini.
Mihimili Mitatu
Tumerithi utaratibu wa uendeshaji wa nchi kupitia mihimili mitatu ya Serikali, Bunge, na Mahakama toka kwa Waingereza. Utaratubu huu una kanuni zake. Sisi tumeiga uendeshaji tuu lakini hatufuati kanuni zake.
Mhimili hii inaongozwa na wakuu wa mihimili, Serikali ikiongozwa na Rais, Bunge likiongozwa na Spika, na Mahakama ikiongozwa na Jaji Mkuu.
Kila mhimili una kazi zake, majukumu yake, mamlaka yake, madaraka yake, na mipaka yake, ambayo haipaswi kuingiliana. Kwa mujibu wa muundo wa mihimili hii kinadharia, mihimili hii inapaswa kuwa sawa, (equal), hakuna mhimili mkubwa wala mhimili mdogo, yote ina haki sawa.
Mihimili hii inapaswa kila mmoja kuwa huru kutoingiliwa na mhimili mwingine, na kuheshimiama baina ya mihimili katika kanuni inayoitwa kwa kizungu, (The Doctrine of Separation of Powers, Checks and Balance) hii ni kanunu ya kila mhimili kuwa huru lakini pia kila mhimili ni kiranja wa mwenzake. Huu ukiranja wa mihimili Tanzania ni kama haupo!.
Tukianzia na jukumu la Bunge kutunga sheria, sii mara moja wala mbili mnasikia Mahakama imebatilisha sheria fulani kwa kwenda kinyume na Katiba. Hiyo maana yake ni Bunge limetunga sheria batili. Kwa vile kuna kanuni ya mihimili kuheshimiana, Mahakama inabatilisha tuu sheria batili zinazotungwa na Bunge, bila kuliuliza Bunge linawazaje kutunga sheria batili, huku limeshehenezwa na wanasheria nguli, wabobezi na wabebovu?. Ukiranja ungekuwepo, hili lisingetokea!.
Jibu ni moja tuu, Bunge letu halitungi sheria, miswada ya sheria inatungwa na serikali, na kuletwa Bungeni ijadiliwe na kupitishwa kuwa sheria, kitendo cha Bunge kujadili miswada hiyo na kupitishwa, ndiko kunakohesabiwa ni Bunge kutunga sheria.
Hii kwa maoni yangu ni Bunge linatumika tuu kama rubber stempu kuipitisha miswada ya sheria inayotungwa na serikali, hivyo anayetunga miswada batili ni serikali yetu tukufu!. Kutokana na kule kule kuheshimiana kwa mihimili, serikali inatunga muswada wa sheria batili, Bunge linapitisha na kuitunga sheria batili, na rais wetu analetewa sheria batili na kuzisaini kuanza kutumika!.
Katika hili la Bunge kutunga sheria batili, sheria ya uchaguzi iliyopita ilikuwa ni sheria batili, kwa kwenda kinyume cha katiba. Mahakama Kuu ikaibatilisha, serikali ikakata rufaa kupinga kubatilishwa huko, ikashindwa, serikali ikapeleke Bungeni, mabadiliko batili ya katiba kwa hati ya dharura, na kukichomekea kiubatili kipengele batili, ndani ya katiba yetu, ili kuihalalisha ile sheria batili kuwa ni sheria halali, kwasababu sasa iko rasmi ndani ya Katiba yetu!.
Mahakama Kuu ikaigomea serikali kwa kushikilia msimamo kuwa sheria ya uchaguzi ni batili, na mabadiliko ya katiba, yaliyofanywa na Bunge, kuichomekea batili hiyo ndani ya katiba, pia ni batili!. Kitendo cha kuichomekea batili ndani ya katiba yetu, na sawa na kuinajisi katiba!.
Serikali ikakata rufaa Mahakama ya Rufaa, na kesi kusikilizwa na majaji watu, kisheria inaitwa (half bench), Mahakama ya Rufaa, kwanza ikaunga mkono uamuzi wa mahakama kuu kuwa sheria ya uchaguzi ni batili, na mabadiliko ya katiba yaliyofanywa na Bunge, kuichomekea batili hiyo ndani ya katiba yetu pia ni batili. Ndipo serikali ikaomba kufanya mapitio, Mahakama ya Rufaa, ikakaa na majaji 7, (Full Bench) chini ya Jaji Mkuu mwenyewe wa wakati huo. Tena Mahakama ya Rufaa, haikukaa peke yake, ikawaita mabingwa watatu wa sheria kuwa marafiki ya mahakama (amicus curiae).
Mahakama ya Rufaa, ikatoa uamuzi kwa kusema “The court is not the custodians of the will of the people! But the parliament” kumaanisha mhimili wa Mahakama sio mlinzi wa matakwa ya watu, huo ni wajibu wa Bunge”.
Huku ndiko mimi ninako kuita ni Mhimili wa Mahakama kuligwaya Bunge!. Japo ni kweli Bunge ndicho chombo kikuu cha uawakili wa wananchi, lakini Mahakama ndio the custodian wa katiba ya nchi, kumaanisha Mhimili wa Mahakama ndie mlinzi wa katiba, mwenye jukumu la kufsiri katiba na sheria.
Kitendo cha Bunge litunge sheria batili kinyume cha katiba, kisha lifanye mabadiliko batili ya katiba,liuchomekee ubatili ndani katiba yetu ili kuihalalisha ile sheria batili kuwa ni sheria halali kwasababu sasa iko ndani ya katiba yetu, hakikupaswa kuachwa hivi hivi.
Badala ya Mahakama ya Rufaa kuangalia ubatili wa katiba na ubatili wa sheria uliofanywa na Bunge, Mahakama kama mamlaka pekee ya kutafsiri sheria, ilipaswa kuliamuru Bunge, kuwa halina uwezo wa kutunga sheria batili wala uwezo wa kufanya mabadiliko batili ya katiba.
Kitendo cha Mahakama ya Rufaa kulirudisha hili suala Bungeni, Bunge ndio liuondoe huo ubatili, kimepelekea ubatili huo kuwa bado ungalipo ndani ya katiba yetu mpaka leo ninapoandika hapa na hii sheria yetu mpya ya uchaguzi iliyotungwa mwaka huu, umekitumia kipengele hicho batili, hivyo tumetungiwa sheria mpya ya uchaguzi yenye ubatili ule ule, ulikwisha batilishwa na Mahakama.
Bunge litimize wajibu wake kikamilifu ikiwemo kutunga sheria, kuisimamia serikali na kuiheshimu Mahakama, na Mahakama itemize wajibu wake kikamilifu, iliheshimu Bunge, isiliogope, Bunge linapovunja Katiba, Mahakama iliamuru na sio kulibembeleza eti liondoe ubatili wa katiba na sheria, ni liamriwe liondoe.
Paskali.
Rejea

Similar Discussions
- Bunge Letu Kibri na Jeuri ni Bunge Kweli la Kutunga Sheria au ni Bunge Ruber Stemp ya Serikali?. Kwanini Linaogopwa Hivi na Mhimili wa Mahakama?.
- Je, Bunge Linaidharau Mahakama na Kuwadharau Watanzania? Kitendo cha Bunge Kutunga Sheria Batili Iliyoshabatilishwa na Mahakama Kinamaanisha Nini?
- Asking Aloud: Rais Samia anajua Katiba yetu ni batilifu, na Sheria mpya ya uchaguzi aliyosaini ni sheria batili kinyume cha katiba?
- Wajua Kuna Sheria Halali, Batili na Batilifu, Ndoa Halali, Batili na Batilifu, Je Wajua Katiba ya JMT ni Batilifu?. Why Ubatili Huu wa Katiba Yetu?!
- Serikali, Bunge, Ziheshimu Mahakama! Kwanini Serikali na Bunge Hazijatekeleza Hukumu ya Mahakama kuhusu Ubatili wa Katiba na Sheria ya Uchaguzi