Ukiona familia inakosa mkuu wa familia inavyokuwa ndo nchi hii iliko sass. Ambaye angedhaniwa kuwa kiongozi ndo huyo wa msoga lakini kwa matendo yake yeye mwenyewe anajishtukia, anajua siku akisimama kuongea kuna watu wataamsha hasira kwake na kwa familia yake. Kimsingi wananchi wana hasira naye ya kiwango cha juu sana
Kwa sasa wenye kusikia na wasikie, chama hakuna mkubwa wala mdogo na uzuri kila mtu anajiona anaweza, muda wa wazee nao umeisha na hata sauti zao haziwezi tena kwa nyakati tulizopo
Nakumbuka 2010-2015 huyo huyo msoga alikuwa ameshakizika chama kwa style hii kama ya bibi huyu chupu chupu akaletwa mwamba ndo kiasi akawarudishia watu imani na hata mtaani wadau tukaanza tena kuvaa sare zetu. Sasa kwa mara nyingine tena JK yuko nyuma na hawajari hari na kelele za wananchi mtaani. CCM haitakufa lakini mara hii tutaonja shuruba. Na mie natamani hii minyukano izidi kwa manufaa ya Taifa la Tz