Benson Mramba
JF-Expert Member
- Oct 29, 2013
- 766
- 1,884
CCM angalieni mnapopeleka Taifa....Video hizo 2 za usiku ni wananchi wa jimbo la Kongwa wakishangilia msiba......dah,imagine wa mtu ambaye angekuwa Mbunge wao na alikuwa Mbunge wao wa muda mrefu.Mwl Nyerere aliwahi kusema dhambi ya ubaguzi ni sawa na kula nyama ya mtu huwezi kuiacha.
Pia Mwalimu alisema kinachowafanya Watanganyika kusema sisi Watanganyika ni uwepo wa Wazanzabar, na kinachowafanya Wazanzibar kusema sisi Wazanzibar ni uwepo wa Watanganyika.
Aidha Mwalimu alisisitiza atakayeanza dhambi ya ubaguzi kati ya Watanganyika au Wazanzibar hatabaki salama dhambi hiyo itamtafuna haitamwacha salama.
Maneno haya ndio yanayowatafuna CCM kwasasa kwa maoni yangu. Baada ya CHADEMA kususia uchaguzi kwasababu ya ubaguzi wa CCM dhidi yao sasa dhambi ya Ubaguzi inawatafuna CCM wenyewe kwa wenyewe. CCM wamegundua kuwa kumbe ndani yao kuna Wanamtandao, sukuma gang na CCM halisi. Sasa wanashughulikiana.
Uzuri ni kuwa nguvu ileile na mbinu zile zile ambazo zingetumika kuwashughulikia Chadema ndizo hizohizo wanazotumia kushughulikiana wenyewe kwa wenyewe.
Sote ni ndugu Watanzania tusibaguane tufanye siasa safi na za kistaarabu.
Kwa ccm wakitafunana acha watafunane kwani ndio waasisi wa huu ubaguzi,wakikaribia kumalizana wataamka kutoka usingizini na kukemea ubaguzi,na wataitamka haki na usawa na sii tena neno amani huku wakiwashikia wengine mapanga mgongoni.Mwl Nyerere aliwahi kusema dhambi ya ubaguzi ni sawa na kula nyama ya mtu huwezi kuiacha.