Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,750
Kila nikikaa najiuliza kama hawa CCM wapo tayari kuipokea habari ya kushindwa ,maana habari ya kushindwa itaanzia kwenye Bunge la katiba na kuendelea kuwa mtiririko hadi kisinyae na kutokujulikana kama kitabaki kuwa chama cha upinzani au kitakufa.
Wasiwasi ambao umetanda je CCM watakubali kushindwa au watarusha vichwa ? CCM haijazoea kushindwa ,haijazoea kubeba aibu ya kushindwa kitaifa ,kauli za CCM sio za kibusara zimejaa ubabe hawajawahi kuwambia wanachama wao wakubali matokeo kwa jinsi hali inavyokwenda.
Tunawasikia watu haswa waCCM wakielekeza shutuma kwa vyama vingine kuwa vinataka kuivuruga nchi ,vinataka kuleta vurugu na shutuma nzito hata kuhusisha na ugaidi na wafuata upepo nao huamini ,yote yanasukumwa huko na CCM ili kuonyesha dunia kuwa vyama hivyo vina agenda ya siri vinaposhindwa au vitakaposhindwa ,na huhusisha hata hisia za mikutano ya vyama hivyo vinapozungumza kwa sauti kuu na yenye msisimko,tunaona Chadema wanaambiwa hivyo,CUF waliwahi kuambiwa hivyo hata mapanga yao kuonyeshwa kwenye vyombo vya habari na hata UAMSHO nao wamefikia hata kufungwa ,zot hizi ni hila za kuwaonyesha kuwa wapinzani ni waliokusudia kuivuruga Nchi.
Narudia kusema na kuuliza kama CCM wapo tayari kuikubali hali ambayo inawaelekea ya kuanguka ,je wao sio watakaokuwa wa mwanzo kuitia nchi kwenye vurugu na isiyotawalika ?