Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanadodi
Nimesikia nia ya kuandaa mdahalo wa wagombea uenyekiti Chadema.
Huu ni uzi wa swali la ushauri wa bure kwa Chadema, Je wakubali au wasikubali mdahalo wa wagombea Uenyekiti wa Chadema?. Wenzenu CCM huwa hawakubali midahalo!.
Kwa sisi tuliosoma zamani, tulikuwa tunafundishwa midahalo kwenye school debates, nimebahatika kusoma sekondari moja na Tundu Lissu mimi nikiwa A level, yeye O level ila alikuwa mzuri kwenye school debates akitugalagaza hadi sisi kaka zake wa A level!, hivyo ukimuweka Tundu Lissu ambaye ni akili kubwa kwenye mdahalo na akili ndogo, ujue hiyo ni suicide mission kwa huyo huyo akili ndogo!.
Ili mdajalo uwe mzuri, lazima wadahiliwa wawe ni watu wanaolingana lingana kwa sifa kwa kuwa na watu ambao ni like variables.
Huwezi kuwadahilisha wadahiliwa wawili wenye sifa tofauti
Huwezi kufanya mdahalo huku mdahiliwa mmoja ni akili kubwa, akili chemka, mwingine ni akili ndogo, akili lala, automatically akili kubwa itamgalagaza akili ndogo!. Je mtakubali?
Huwezi kufanya mdahalo kati ya mtu mmoja ni mstaarabu, gentleman, mtu mwenye shukrani , anayezungumza kwa lugha ya kiungwa na kistaarabu na kuzungumza vitu vya kweli, ukamuweka na mtu roporopo, mpayukaji anayezungumza uzushi kwa lugha kali, asiye na breki ya ulimi, anaweza kupayuka uongo na uzushi wowote na kuwaaminisha watu uongo huo ni ukweli!, ataishia kumdhalilisha tuu bure huyo mstaarabu wenu!, je mtakubali?
Huwezi kumshindanisha mtu mpambanaji wa kweli, aliyekipigania Chadema kwa machozi, jasho na damu, ikiwemo kumiminiwa pyu pyu 38, 16 zikampata! ukamlinganisha na mtu aliyekabidhiwa chama kama sadaka kwenye kisahani cha chai na Ba Mkwe hivyo kujiona kama chama ni mali yake binafsi, huu ukiwa ni mwaka wake wa 20 kwenye uenyekiti na bado anataka kuendelea tena!, je mtakubali?.
Hivyo hili ni swali la ushauri wa bure kwa Chadema, je mtakubali au msikubali mdahalo wa wagombea Uenyekiti wa Chadema?. Wenzenu CCM huwa hawakubali kabisa midahalo!.
Kwenye uchaguzi mkuu wa 2010, TBC chini ya Tido Mhando ilianzisha kipindi cha Mchakato Majimboni, kilichofanya midahalo ya wazi ya wagombea ubunge, kikiendeshwa na Shabani Kissu, kila jimbo ambalo kipindi kile kilipita, CCM ilipigwa chini!, Elections 2010 - Mchakato Majimboni: JJ. Myika, Ubungo Yako, Njia Nyeupe hivyo baada ya uchaguzi ndio ikabidi Tido ndio vile tena!. Hivyo CCM hawakubali mdahalo wowote wa uchaguzi.
Tuwashauri vizuri Chadema, je wakubali au wasikubali mdahalo wowote wa wagombea Uenyekiti wa chadema?.
Hoja hii nimeileta haswa kwa kuzingatia wengi wa mashabiki, wafuasi, wanachama na viongozi wa Chadema, wana akili kama za yule mnyama nyumbu, wakiambiwa chaguo la chama ni kuendeleza usultani na mgombea wao ni Sultan Mbowe, wao wanasubiri tuu tarehe 20 January, kura zote kwa Sultani Mbowe, hivyo kukifanyika mdahalo kumhusisha Kamanda Shujaa Lissu na Sultan Mbowe, Lissu akamgaragaza Sultani wao kwenye mdahalo, kuna hatari akili za mnyama nyumbu zikawahama, akili za kibinadamu zikawarudia, watamtosa Sultani Mbowe na kumchagua kamanda Lissu, ambaye atawaingiza ikulu 2015!, manyumbu wao hawana haja na ikulu, furaha yao ni sultani wao tuu kwenye kiti cha usultani hata kama watakuwa wapinzani milele!.
Mimi nimewafanyia a comparative ya assets & liabilities za kuiingiza Chadema ikulu, Japo Lowassa Alikuwa a Liability CCM, Akawa Asset Chadema. Lissu is a Very Bad Liability, but is The Only Asset Chadema Has Kuwangiza Ikulu!. Je... ? hivyo kama Chadema wanataka kuingia ikulu, mtu wa kuwaingiza ni Lissu, wala hahitaji mdahalo na yeyote!, lakini kama lengo ni kuendelea kubunya tuu ruzuku, waendelee na Sultani wao.
Haya mambo ya vyama vya kubunya tuu ruzuku, nilishauri Ruzuku kwa vyama vya Siasa: Mnaonaje tumshauri Rais Magufuli aifutilie mbali ruzuku hii? Ni ufisadi, nikashauri Kuelekea 2025 - Pascal Mayalla: Vyama vya siasa visipewe ruzuku, viongozi wake wajitolee
View: https://youtu.be/kpOuytUa4O4?si=0CEA3qzDha1b5_HQ
Amini usiamini, ruzuku kwenye vyama vya siasa ikifutwa, Sultani asinge endelea kung'ang'ania madaraka mwaka wa 20 sasa!.
Namalizia kwa lile swali la msingi la uzi huu, Je tuwashauri Chadema wakubali au wasikubali mdahalo wa wagombea Uenyekiti wa Chadema?.
Paskali.