Je, CHADEMA wanao mbadala mwingine pembeni ya kususa?

Je, CHADEMA wanao mbadala mwingine pembeni ya kususa?

ubongokid

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
2,154
Reaction score
4,184
Huku duniani kuna mifumo mingi sana ya kuondoa tawala yoyote ile madarakani,Baadhi ya njia hizo ni halalai na nyingine ni haramu.

Katika kutafuta haki unaweza kuamua kutumia njia halali au kuamua kutumia njia haramu yote inategemea tu na malengo yako kisiasa.

Je, ni kweli Chadema wamesihiwa kabisa na mikakati mpaka wameamua sasa kususa?Wamewachoka watanzania?Ni waoga?Hawana pesa?Hawana nguvu,Hawana watu? Wameshindwa kabisa kutafuta njia mbadala ya kuleta mabadiliko katika nchi hii?

Je, Chadema nao wanalo tatizo la Ombwe la uongozi?Je wanafanya maamuzi kwa mihemuko?Je Chadema impeoteza ushwawishi hapa Tanzania?Je ina maana kwamba sasa watanzania watafute chama mbadala?Je watanzania waamue kutumia mbinu mbadala ili kupata haki wanayoitaka?

Nani aliwaambia Chadema kwamba kususia uchaguzi ni suluhu?

Binafsi ninachokiona ni kwamba chama kimeshindwa kabisa kufanya organaizesheni kuhakikisha kwamba kila kitu kinakwenda swa na badala yake kinaishi kulia kwamba wanachezewa rafu.

Chadema pamoja na viongozi wote,mnajua kwamba mnachezewa rafu kwa nini na nyie hamchezi rafu?Mnajua kwamba CCM wanawachezea shere kwa nini na nyie msiwachezee shere?Kama hamjui kucheza rafu basi acheni kulia lia kwani ni UMAMA

Kususa kwenu kuna wapa CCM fursa ya kuendelela kuwashikia chini mpaka ikifika 2020 mtajikuta mko hoi hata raundi ya kwanza mtashindwa.

WITO WANGU NI HUU;

KAMATI KUU YA CHADEMA ITENGUA UENYEKITI WA MBOWE ILETE DAMU MPYA KOROFI NA ISIYOJALI AMBAYO ITAWAJIBIKA KATIKA KUIVUSHA CHADEMA ISIJE KUFA KAMA KIBUDU

Nimemaliza kama unacho cha kuchangia karibu kama huna soma halafu upite hivi
 
Tatizo tulizoea siasa za ulaghai Amekuja Mzalendo Magufuli yeye ni kutenda Sio kuongea



Mtakuja kuelewa kwamba Magufuli Ni jiniasi mkiwa mmeshasambaratika

Badilisheni aina ya siasa mnazofanya

Magufuli is there for more years to come
 
Tatizo tulizoea siasa za ulaghai Amekuja Mzalendo Magufuli yeye ni kutenda Sio kuongea
Mtakuja kuelewa kwamba Magufuli Ni jiniasi mkiwa mmeshasambaratika
Badilisheni aina ya siasa mnazofanya
Magufuli is there for more years to come
Sina haja kusoma comment yako maana najua ni upupu tu.
 
Magufuli ni moto wa kuotea mbali. Mlidhani mtaleta nyodo mlizokuwa mnamletea mkwere anawachekea? Magufuli kawasoma kuwa hamjui sheria pia CHADEMA woote vilaza. Mmeshindwa kufuata katiba ya chana chenu kumuondoa Mbowe kwenye uwenyekiti wakati muda wake uliisha kitambo ndo muje kukiondoa CCM madarakani? Kujaza form tu za kugombea uwenyekiti wa serikali za mtaa mmeshindwa alafu eti mnazila na kugonea uchaguzi. Kagomeni CCM itaendelea kutawala milele. Magufuli anacheza na akili zenu mbovu
 
Jamaa hawajajifunza hata kwa kilichotokea Zanzibar pale CUF ilipoamua kuondoka mezani na kuachia ccm ugali wote.
 
kila mtu anajifanya mjuaji na kuhoji 'hakuna njia mbadala' lakini na ninyi hamsemi hiyo njia mbadala ni ipi! huu ni upumbavu, mnataka chadema waingie msituni? vyama vya upinzani havitetei matumbo yao bali vinatetea ustawi wa demokrasia, utawala bora, uwajibikaji na maendeleo ya wananchi. mnufaika mkuu wa mapambano ya vyama hivi ni mwananchi, sasa basi wananchi ndio mwenyejukumu la kusema tumechoka kuonewa na utawala huu, tunaung'oa kwa jasho na damu.
acheni kuandika lawama za kipimbavu.
 
Back
Top Bottom