Pre GE2025 Je, CHADEMA wapo tayari kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

LAZIMA NISEME

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2015
Posts
240
Reaction score
267
Na Mwandishi Wetu

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), katika kipindi hiki ambacho nchi inajiandaa kwenda katika uchaguzi wa serikali za mitaa kimejipanga kuvuruga uchaguzi lakini pia ionekane nchi haina demokrasia na haitawaliki.

Ni kama kwa muda mrefu wamekuwa wakiitafuta fursa hii lakini hawakujua wapi pa kuanzia, hata baada ya kuzuiwa mkutano wao wa vijana kuadhimisha siku ya vijana duniani jijini Mbeya, ambapo mkutano huo uliandaliwa na Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA) mnamo Agosti 12, 2024.

Mgeni rasmi alitarajiwa kuwa Makamu Mwenyekiti Bara, Tundu Lissu ambaye aliambatana na viongozi wengine wa kitaifa na kikanda kwa Kanda ya Nyasa. Wakiwemo Katibu Mkuu wa chama hicho John Mnyika na Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu.

Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA, Moza Ally katika moja ya kauli zake alisikika akisema:

“Kama kijana yeyote unayeipenda nchi yako ya Tanzania umeshalia miaka yako yote, siku hiyo ya Agosti 12, 2024 tunakwenda kuweka hatma ya taifa letu la Tanzania mkoani Mbeya, kwa hiyo kijana yeyote uliyepo popote Tanzania njoo Uwanja wa Ruanda Mzomve, Mbeya.

“Tupo Serious na jambo hili, kwa hiyo vijana wote wa CHADEMA kama ambavyo vijana wa Kenya wamejitambua siku ya Tarehe 12/08/2024 tunakwenda kuacha uteja kwa serikali, vijana wa Kitanzania na kuweka maazimio makubwa ya uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwaka 2025.”

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo Jeshi la Polisi Tanzania, Awadh Juma Hajji alitimiza wajibu wake kuzuia mkutano huo. Baada ya viongozi kukaidi likaingilia kati na kuwadhibiti John Mnyika, Tundu Lissu na Joseph Mbilinyi.

Kwa madai yao yasiyo na uthibitisho wowote wanadai wakiwa chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi jijini Mbeya waliteswa na kuumizwa, huku siku ya leo (Jumatano Agosti 14, 2024) zimesambaa picha za Joseph Mbilinyi ambaye anaonekana yuko kwenye kitanda cha hospitali amelazwa.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ameita wanahabari jijini Dar es Salaam kuzungumza nao. Lakini ni wazi wanatafuta huruma kwa mataifa ya nje ili ionekane nchi haina demokrasia.

Itakumbukwa Januari 2023, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan aliwaita viongozi wa vyama vya siasa vyenye usajili nchini kikiwemo CHADEMA katika Ikulu ya Magogoni jijini Dar es Salaam.


Mbali ya mambo mengine Rais Samia aliruhusu mikutano ya vyama vya siasa kufanyia kwa uhuru popote nchini. Akazungumzia kuhusu R4 ikiwemo kurudisha mahusiano mazuri baina ya serikali vya vyama vya siasa.

Yote hayo hayaonekani kama ni moja ya mambo muhimu kwa nchi kuendelea, bali kinachotaka kufanyika ni kuvuruga kazi kubwa iliyofanywa na Rais Samia tangu aingie madarakani.

Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika, CHADEMA wanataka kufanya maandamano makubwa jijini Mbeya katika siku za hivi karibuni.

Pia wanataka kuvunja maridhiano yaliyowekwa na serikali kwa vyama vya siasa walipokutana Januari 2023. Kwamba iwe iwavyo, vurugu zitokee, Jeshi la Polisi liingie mtaani kuwadhibiti, wananchi wasio na hatia waumizwe, wafanyabiashara waibiwe vitu vyao na watu wasio na nia njema, nchi iwe haikaliki.

Zaidi ya hayo wanataka kutafuta huruma kwa mashirika ya kimataifa ili wawapeleke viongozi wao nje ya nchi kwa matibabu kwa sababu ionekane nchini hakuna haki.

Bila kuzingatia kuwa kwa sasa mataifa jirani yanakuja nchini kufuata matibabu ya kibingwa kwa sababu ya hospitali za kisasa zenye vifaa vya hali ya juu vya matibabu hivyo hakuna sababu ya kutibiwa nje ikiwa kweli wameumizwa.

Wananchi lazima waamke, wajue kuwa viongozi hawa hawana nia njema na nchi yetu. Vile vyama vya ukombozi vilivyowika katika miaka ya mwanzoni mwa 1950 hadi mwishoni mwa miaka ya 1980 vingi vimepotea, havikupotea kwa bahati nasibu bali vimepotezwa na hao wanaoitwa mashirika ya kimataifa.

Chama kilichobaki imara hadi sasa ni Chama Cha Mapinduzi (CCM), hivyo nia ni kuhakikisha na hiki kinapotea.

Wamejaribu njia nyingi ikiwemo kuwalaghai wananchi wakati wa uchaguzi, lakini raia wa Tanzania bado ni watu wenye akili na busara. Wanajua kipi sahihi na kipi si sahihi.

Hivyo, CHADEMA watafute mbinu nyingine ya kuwahadaa wananchi lakini si kuanzisha vurugu na kuirudisha nchi shimoni. Watu walishasahau kuingia barabarani kuvutana na Jeshi la Polisi. Nchi ina amani na uchumi wake ni imara, wachache tusiwape nafasi ya kutuvuruga.
 
Nafikiri wa kuwauliza ni CCM kwamba wapo tayari kushindana kwa haki?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…