DOKEZO Je, Chuo cha Tabora Polytechnic kilichopo Tabora mjini kimeuziwa taarifa za wanafunzi na Ndono Sekondari?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Waulizeni vizuri watoto zenu.


Wengi wao hupendelea kwenda chuo hivyo wakati mwingine hufanya application pasipo wewe kujua. Kumbuka hao jamaa wanafanya matangazo Sana.

Pia Wanafunzi Ni Kama nyumbu.
 
Kuna mfumo unatumika kupata majina na namba zao kwa wanafunzi walio maliza form four.

Ukinipa jina la shule uliyo maliza pamoja na mwaka nitakupatia majina ya uliohitimu nao pamoja nawewe ukiwemo mbona ni kitu cha kawaida.
 
Na Tabora boys pia ni kesi hiyo hiyo. Hiki chuo kichunguzwe pamoja na shule tajwa. Wanatibua sana Wazazi huku mitaani. Ni wapumb*vu sana.
 
kuna mfumo unatumika kupata majina na namba zao kwa wanafunzi walio maliza form four. ukinipa jina la shule uliyo maliza pamoja na mwaka nitakupatia majina ya uliohitimu nao pamoja nawewe ukiwemo. mbona ni kitu cha kawaida.
Huo mfumo nani castodian? Anaruhusiwa kuzitumia hizo taarifa katika mazingira yapi? Haya ndio mambo yanayohojiwa mkuu.
 
Reactions: G4N
huo mfumo nani castodian? Anaruhusiwa kuzitumia hizo taarifa katika mazingira yapi? Haya ndio mambo yanayohojiwa mkuu.
Kwani ndugu, ulipopewa jina Kuna conditions ziliwekwa za mazingira yapi na watu gani wanaruhusiwa kutumia jina lako?

Uliposajili namba yako ya simu, Kuna conditions ziliwekwa za mazingira yapi na watu gani wanaruhusiwa kutumia namba yako ya simu?

Ulipoingia shule, ukapewa namba ya mtihani, Kuna conditions ziliwekwa za mazingira yapi na watu gani wanaruhusiwa kutumia namba yako ya mtihani?

Kama hizo conditions hazijawekwa, unaanzaje kulaumu taasisi zinazotumia majina na namba za simu kutangaza nafasi za masomo?

Andaa conditions kwanza, nenda kwa mwanadheria, then toa matangazo, Kisha Anza kulaumu na kuwachukulia hatua wale watakaotumia jina na namba zako kinyume na matakwa yako
 
Watanzania mtaacha kutapeliwa mpaka lini?
Mbona kila siku tunatumiwa sms kuwa umeshinda hujiulizi namba wamepata wapi.
Kama umetumiwa sms hiyo achana nao kama hukiamini chuo utatapeliwa.
 
Hiki chuo Cha Tabora polytechnic (T.P.C) a.k.a Musoma utalii,hawajaacha utapeli,juzi Kuna mwanafunzi Mmoja ametapeliwa 380,000/= na mwalimu Mmoja anaitwa Kizwalo,mbaya zaidi inaonesha baadhi ya viongozi unashiriki huu utapeli,Yaani kile chuo ni utapeli kwa kwenda mbele.
 
Kuna vyuo vya afya vya binafsi viko juu ya sheria.Pesa inawaweka juu ya sheria na hawagusiki.
Mfano wa vyuo hivyo ni hicho ulichotaja,na vingine vimejaza mabango nchi nzima.

Vyuo vinawatu wanasaka mitihani kwa udi na uvumba ili waendelee kuwa na idadi kubwa darasa lenye zaidi ya watu 300 huku idadi ya wakufunzi ikiwa ni ndogo.
Hivi vyuo vimeshakuwa sugu kama chama tawala.
 
Watanzania mtaacha kutapeliwa mpaka lini?
Mbona kila siku tunatumiwa sms kuwa umeshinda hujiulizi namba wamepata wapi.
Kama umetumiwa sms hiyo achana nao kama hukiamini chuo utatapeliwa.
Mm siku hz wale wa tuma kwenye namba hii narudisha sms ya tusi tu, nshachoka mie.
 
TAPEL JINGINE HLI HAPA
 
Reactions: G4N
Ukitaka kujuta maisha yako yote nenda au mpeleke mtu asome hapo TPC
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…