Stevenbee
JF-Expert Member
- Oct 16, 2016
- 365
- 449
Habari zenu wapendwa natumaini mpo wazima wa Afya,
Kama kichwa cha habari kinavojieleza hapo juu kuhusiano na ugonjwa wa uviko ulioanza mwanzoni mwa 2020 kwa Tanzania.
Kwanza ningependa kufafanua kwanini nimeuliza swali la namna hiyo?
Naomba tiririka na Mimi katika kisa hiki kifuatacho.
Nilimaliza chuo mwaka wa 2019 na nikarejea nyumbani, Dar-es-salaam, na muda huo wote nilikuwepo tu nyumbani nafanya shughuli za hapa na pale na kipindi Cha February tulianza kusikia juu ya ugonjwa huu kuwepo nchini Tena kwa tahadhari kubwa Sana na takwimu zilitolewa! Na tukawa tunavaa Barakoa.
Bahati nzuri sna rafiki au jirani ambaye alipatwa na athari za huu ugonjwa.
Siku moja shemeji Yangu alirudi nyumbani anakohoa sana, alitumia dawa kwa ajiri ya kikohozi lakini wapi,alienda hospital fulani akaambiwa ni allergy wakampa dawa za allergy na kumuagiza atumie sana limau na maji ya Moto na kujifukiza, alitii masharti Basi Kama familia wote tukaunga tela la kupata kikombe kimoja kimoja cha mchemsho wa limao pamoja na tangawizi mwishowe alikuja akawa yupo vizuri tu, siku moja Mimi nilitoka nikaenda sehem fulani hapa hapa Dar-es-salaam, nilianza kujisikia Kuchoka sana kwakuwa nilikuwa kwa rafiki Yangu nikalala ilikuwa mchana.
Nilipoamka nikajisikia afadhari kidogo, nikapanda Daladala na kurudi nyumbani wakati huo nimevalia barako,ila gafla nilianza kuishiwa pumzi bahati nzuri nilikaa dirishani nikafungua dirisha na kuvua barako, nilipofika kwenye kituo changu nikashuka ila nikajiona siwezi kabisa kutembea kutoka pale mpaka nyumbani ingawa huwa natembea nikachukua pikipiki baada ya kufika nyumbani nikachukua hela nikaenda pharmacy kupima wakanambia nina malaria pamoja na allergy kwakuwa nlikuwa nina Kama dalili za mafua huku kichwa kinauma.
Basi nikarudi nyumbani nikaanza hiyo dozi ya mseto baada ya kuimeza niliumwa kichwa vibaya mno siku ile nikalala kufika kesho asubuhi nilikuwa nina dalili tosha za kuumwa ila kitu nilichoshangaa sikuwa naweza kusikia harufu ya kitu Chochote,hata nikienda chooni sisikii chochote, niliapa kuachana na dozi ya malaria nikaendelea kunywa limau, tangawizi na maji ya Moto kwa wingi,baada ya siku mbili mdogo angu nae akawa hasikii harufu. Mara bi mkubwa ikawa nyumba yote (watu 6) Mimi binafsi sikujua ni nini ukienda hospitali unaambiwa mchafuko wa hewa mtapona tu,Basi tukaendelea kupiga mchemsho baada ya wiki na siku kadhaa nilianza kurudisha harufu kwa umbali huku mwili ukianza kujisikia vizuri,baadae nilianza Mimi kupona,akaja bi mkubwa, mdogo angu na wengine tulikuwa tupo tu nyumbani mda wote.
HUENDA TULIPATWA NA CORONA
Okay kwa kipindi Hiko chote sikuwahi kujua Ni Nini kilitupata,kwakuwa Kila mtu tulipata dalili zinazofanana hususani kutokusikia harufu,kupumua kwa shida usiku na mwili kuwa mchovu,siku moja nilienda chuo kuchukua cheti nikakutana na Dada mmoja na yeye kwa maongezi yake akasema walipatwa na hali hiyo hiyo na wao waliambiwa mchafuko wa hewa unaendelea Dar-es-salaam walihangaika na mchemsho wakapoana tukiachana na huyu siku nikapata smartphone nikaangalia dalili za ugonjwa (covid-19) nikaona nilipata dalili karibia zote za ugonjwa husika pamoja na wanafamilia wenzangu nilishangaa Sana, ikawa siri yangu tu baada ya kujua hilo, siku moja nikiwa Facebook, kuna dada aliandika kuwa tujikinge na corona,nikamfata inbox kumuuliza kwa Nini? Na yeye akajibu alipata Dalili fulani fulani (zinazoendana na Hizo nilizopata) akaambiwa na Dada yake kuwa Ni corona kwakuwa hata Dada yake alipata akapima akajibiwa hivo, nikastuka kidogo na nikapotezea tu
Kwanini huu ugonjwa huenda usiwe hekaya? Au hadithi Kama wengi wanavodhani?
Kati ya rafiki zangu kumi Ni mmoja tu anaamini uwepo wa huu ugonjwa, na wanasema ni kwa ajiri ya wazungu na wenye pesa, nikiwatolea ushuhuda wangu wanasema si kweli🖐️ Sio kosa lao hata Mimi pamoja kwamba nilipatwa na dalili za huo ugonjwa bado simuamini mpaka nilipopata uthibitisho kutoka kwa watu tofauti tofauti!
Dalili nilizokuwa nazo
1) Kutokusikia harufu ya kitu chochote
2) Kichwa na uchomvu
3) Kupumua kwa shida hasa usiku
4) Radha ya chakula hakuna
4) Mwili kutokuwa sawa
Juzi nimepiga stori na bi mkubwa nikamkumbushia Hilo sakata akajibu "Ah ile ilikuwa corona tu,Hivi hukuona shemeji yako alivohangaika kile kifua, na sisi wenyewe? Sema tulikuwa tunajikaza tu tutoe hofu kwa watoto".
Kama umeokota kitu nijibu kwenye hapa chini👇