JE CRDB hawataki kukopesha?

JE CRDB hawataki kukopesha?

herrera

Senior Member
Joined
Jul 30, 2017
Posts
108
Reaction score
260
Wakuu kama kuna mtu wa crdb humu au mwenye taarifa kamili naomba atujuze hili suala.

Mimi ni mtumishi wa serikali nilifanya maombi ya mkopo toka jumatatu kupitia mfumo wa ess ila maombi yakawa yamekwama level ya service provider ku accept ili afisa utumishi aweze kuona na kupitisha, kesho yake (Jumanne) nikawapigia kakapokea kadada flani kanaitwa Neema (kana nyodo balaa) nilipo kaelekeza shida yangu kakaniambia kuwa mvumilivu tuna shughulikia then kakata simu bila hata kuuliza details zozote,

Nikaona anyway ngoja nijaribu kuingia kwenye magroup ya wafanyakazi wenzetu wa taasisi moja nijaribu kuulizia kama nitapata namba ya Afisa mikopo kwenye tawi nililo karibu nalo, nilicho kutana nacho huko ndio balaa, kuna wengine wanadai wanazaidi ya siku kumi toka wame apply lakini hawajaingiziwa tofauti na bank zingine.

Mfano siku nina apply kupitia mfumo tulikua na wife yeye aliomba Azania, yeye ndani ya masaa 24 hela yake ilikua imeshaingia, saizi natamani kama kuna uwezekano wa ku cancel crdb ni cancel na mimi niombee azania, Hivi crdb mna shida gani tuwekeni wazi basi
 
Ndio ilikua target yangu but nilifeli kufungua account, tabora nzima hakuna tawi la azina
Hazina hpo kila makao makuu ya mkoa wewe haujataka kuulizia. Zinaitwa ofisi ndogo hazina.
 
Back
Top Bottom