Je, CT Scan ya Figo ina madhara? Kuna idadi maalum ya kufanya CT Scan? Majibu yapo hapa

Je, CT Scan ya Figo ina madhara? Kuna idadi maalum ya kufanya CT Scan? Majibu yapo hapa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
JamiiForums iliwasiliana na Dkt. Hellen Makwani, Daktari Bingwa wa Saratani na Tiba Shufaa, ili kufafanua kwa undani madhara yanayoweza kusababishwa na CT scan, baada ya mtumiaji wa jukwaa kuuliza kuhusu athari za CT scan ya Figo - CT scan ya Figo ina madhara?

Mtaalamu wetu alijikita katika kutoa majibu ya kina na ushauri wa kitaalamu kuhusu usalama na manufaa ya kipimo hiki.

1737700216605.jpeg

Picha kwa hisani ya mtandao

Je, kuna kiwango cha CT scan ambacho mtu hatakiwi kuvuka ndani ya mwaka mmoja?

CT Scan ni kipimo kinachoweza kuonyesha mabadiliko ya muda mrefu, ndani ya mwaka, hakuna idadi maalum za kufanya CT Scan, kwa mfano, hata ukifanya uchunguzi mara mbili kwa wiki au mara nne kwa mwezi, inaweza kuwa sahihi kulingana na usimamizi wa ugonjwa wa mgonjwa.

Ingawa maendeleo ya teknolojia kama PES scan (Positron Emission Scan) yameleta njia mbadala. PES scan inaweza kufanyika mara moja kwa mwaka ili kugundua mabadiliko ya awali ya saratani na mara mbili ikiwa ni muhimu kufuatilia mabadiliko kabla na baada ya matibabu.

Je, matumizi ya mara kwa mara ya CT scan yanaweza kusababisha madhara kiafya?

Mionzi ya CT Scan sio mionzi inayoweza kuleta madhara kwa haraka. Hata X-ray pia inahitaji kufanya mara nyingi ili kuweza kuona madhara yake.

Ni wakati gani CT scan inashauriwa kuwa lazima?

Ili kufanya CT Scan, ni lazima upitie vipimo vingine vya awali (kama vile Ultrasound na X-ray). Daktari atashauri kulingana na hali ya mgonjwa. Haiwezekani kwenda moja kwa moja kufanya CT Scan bila kufanya vipimo vya awali. CT Scan itasaidia kufafanua zaidi kile daktari alichokiona.

Kuna njia mbadala na salama tofauti na kufanya CT scan kwa uchunguzi?

Njia mbadala ya CT Scan inategemea eneo la mwili. Kwa mfano, kwa mgonjwa wa Uti wa Mgongo, anaweza kufanya MRI. Hata hivyo, PES scan ni kipimo kipya kinachopatikana katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, ambacho mtu yeyote anaweza kufanyiwa ili kubaini dalili zozote za saratani.

PES scan ina uwezo wa kuonyesha mabadiliko ya awali ya seli za saratani kabla saratani haijajitokeza wazi. Hii ina maana kwamba mtu anayeanza kubadilika kutoka kwa seli za saratani miaka mitano iliyopita anaweza kutibiwa mapema.

PES scan pia hutumika kwa watu waliotibiwa saratani, ili kufuatilia maendeleo ya afya yao.
 
Back
Top Bottom