Precious Diamond
JF-Expert Member
- Jun 9, 2023
- 593
- 1,376
Salam Wakuu,
Kama kawaida msemaji kujiteua kwenye masuala ya maji Mbezi Beach nimekuja na update.
Kwa majibu tuliyopewa na Meneja wa DAWASA Kawe inaonekana kuna mgao. Maana maji yanazuiliwa kwa baadhi ya masaa ili wengine wapate jambo linalofanya baadhi ya maeneo kupata maji kwa presha ndogo sana na wengine ndio tunakosa kabisa. Wizara ya Maji
Kwa maneno haya ni dhahiri kuwa kuna mgao. Waziri Wizara ya Maji toka hadharani utuambie nini kinaendelea, hayo maji unayosema yapo hatuyaoni, na hizo bilioni unazotaja kila siku zinatumika kuboresha miondombinu na matengenezo ya mara kwa mara hatuoni matunda yake.
Wakuu huko mliko hali ikoje? Wekeni hapa na kuwatag Wizara ya Maji wapate notifications za kutosha watupe majibu ya kueleweka.
Hii hapa convo kutoka group la DAWASA Mbezi Beach, hii ilikuwa jana, mtaani kwetu maji yalirejea kwa masaa kadhaa tukarudi kule kule, yamekatwa jana ile ile mpaka sasa naweka uzi huu hayajarudi.
HILI JIBU LA MENEJA HAPA CHINI NI KWAMBA AMETUAMBIA TUPO KWENYE MGAO!
Kwamba ni miezi hii miwili hapa ndio matumizi yamekuwa makubwa ila kabla yalikua hayatumiki sana wakati wa asubuhi? Tumechoka majibu yenu ya kisiasa.
Maji yalijaa mpaka yanamwagika sasa mgao huu umetoka wapi? Wizara ya Maji
====
Majibu ya wadau kuhusu maeneo mengine

Mkuu hiyo sio huko kwenu tu hata Sinza hali ni hiyo hiyo.
Ikishafika tu saa 3 usiku wanakata hadi 6 usiku ndo wanarudisha.
Yaani mtu umetoka kwenye mizunguko yako unataka utulie na familia maji hamna na tangazo hawatoi.
Wizara ya Maji naomba uliangalie hili