Nadhani kwenye hili jina la daraja inafaa kutoka kwenye mjadala mwembamba na kuutanua.
Jina la daraja limeshatolewa. Ila kutakuwa na vitu vingine huko mbeleni.
Kazi ya kutafuta majina ya miundombinu na kumbukumbu iwe mojawapo ya majukumu ya wizara ya Nape. Kuwe na kitengo maalum cha kimkakati cha kuhakikisha vitu fulani havisahauliwi. Itengenezwe waiting list iliyotokana na utafiti.
Kwenye hili la daraja, ni mfamo mzuri wa jinsi tusivyopjipanga na tusivyo na vyombo husika. Tukilipanua ni vema
Fikiria ,unateremka uwanja wa Mwalimu Nyerere, unapitia barabara ya Nyerere, kisha daraja la Nyerere kulekea chuo cha Nyerere, unaamkia mkutano ukumbi wa Nyerere
Kwa watu wanaojua kuenzi na kupanga miji hii ina chosha na kutoa picha isiyo nzuri kwamba Taifa hili ima halina au linaupungufu wa 'mashujaa' au thamani zake za vitu
Tena uwanja wa ndege ungeitwa Nyerere Inter Aiport inge sound vizuri sana kuliko jina Mwalimu Julius Nyerere. Halitamkiki vema hasa kwa wageni wasiojua kiswahili
Daraja la Rufiji limeitwa Mkapa.
Nini nafasi ya watu wa Rufiji katika ukombozi wa Taifa hili?
Je, hatutambui maji maji ilipigwana sana maeneo hayo? Akina Kinjeketile wapo wapi?
Kilimanjaro inter aiport ipo Arusha Zaidi ya Kilimanjaro. Kwa mkakati kabisa ikaitwa Kilimanjaro kwasababu ya Mlima na hivyo kuwa sehemu ya kutangaza kivutio hicho.
Mtu anaye google Kilimanjaro mara nyingi hukutana na K'njaro airport.
Hivyo ndivyo tunaheshimu thamani zetu
Kwasababu mambo haya yanafanywa na wanasiasa wasiojua lolote bali kujipendekeza, leo hakuna anayejua Kichwele au mzizima na kuna kosa gani kwa majina kama hayo?
Wanasiasa wamebadilisha Bagamoyo Rd yenye historia inayotukuka na sasa ni Kibaki. Wamebadilisha ocean Road na sasa ni Obama.
Kwanini Ocean road isiitwe Dr Robert Coch Rd? Huyu ni mwanasayansi aliyetafiti ugonjwa wa TB duniani. Nani anajua kuwa Robert alifanya kazi Ocean Rd?
Je, haikuwa jambo jema ili kuamsha fikra za vijana wa leo kutambua thamani na umuhimu wa maeneo?
Kwa nchi za wenzetu zipo kamisheni maalumu za kutafiti na kutoa majina tena kwa vigezo kadhaa. Si kwamba ni kamisheni za watu kukaa wakisubiri, bali ikibidi watu hao huitwa kutokana na nyadhifa zilizopo.
Mfano, mkurugenzi wa makumbusho(museum), wasomi wa historia, wachambuzi wa masuala ya kijamii, viongozi wa taasisi muhimu za kitaifa n.k.
Hapa sikubaliani na kuwakabidhi akina Mh Nape. Hawa ni viongozi wanapita tu, kinachotakiwa ni kamisheni inayotokana na nyadhifa za watu katika muda uliopo
Kama ni kumuenzi mwalimu, Chuo cha Kivukoni ingekuwa taasisi moja kubwa na pengine kuitwa Nyerere center of excellence.
Ingetosha kuendeleza legacy yake kwa heshima kuliko kutawanya jina lake tuu bila kuwa na maana halisi ya kumuenzi mwalimu
Ukiwauliza waliotoa jina la uwanja wa ndege wa Dar, barabara ya Pugu, daraja la Kigamboni, chuo cha kigamboni na ukumbi wa mikutano kwanini wametoa jina la Nyerere , hakuna atakayeweza kusimama na kutetea kwa hoja na mantiki
Jibu rahisi utasikia ni Rais wa kwanza.
Hakuna anayeweza kutetea jina hilo, huku wakijifanya wana muenzi.
Ndio, wanajifanya kwasababu hawana sababu za kutushawishi wala matinki.