Je, Diaspora wetu wana mchango wowote kuisaidia Tanzania kisiasa? Wana any influence kwenye siasa za nchi yetu? Angalia Diaspora wa India

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Nimesoma mahali kuhusu mchango wa diaspora na influence yao kwenye siasa za nchi zao, hivyo najiuliza, je hawa wana diaspora wetu sisi Tanzania, waliotapakaa ulimwenguni kote, jee wana mchango wowote katika siasa za nchi yetu? Je, wana influence yoyote kutumia their exposure na the economic muscles to help out shaping the political trends za siasa za nyumbani?, au wana diaspora wetu wapo wapo tu?

Angalie diaspora wa wenzetu India, walioko Marekani, wanafanya nini kwa ajili ya nchi yao, je diaspora wetu wanashindwa nini?


Mimi ni interested party ambaye napenda kuona Tanzania tunafaidika na mchango wa wana diaspora wetu wenye exposure kubwa huko walipo, kuitumia kulisaidia taifa letu kisiasa, kiuchumi cha kijamii.

Paskali
Rejea kuhusu diaspora.
 
Pascal Mayalla,

Unawazungumzia hawa akina Nyani Ngabu na Mange au wale aina ya akina le mutuz enzi zao?! Anyway niliifuatilia ziara ya Dr Mahiga kule Sweden kwa Dr Slaa na ile ya Prof Kabudi kule Merekani kwa Masilingi hakika diaspora wetu bado wana uwezo mdogo sana wa kifikra achilia mbali kiuchumi. Ilibidi diaspora wa zamani Prof Kabudi mwenyewe na mwenzie Dr Ryoba wa TBC wawape darasa namna ya kushiriki shughuli za huku nyumbani, ila sidhani kama walielewa maana walionekana " kuchoka".
 
Hawana influence kubwa ila wanatoa mawazo mazuri kuhusu siasa zetu kama tunavyowaona humu JF na raia wengi hujifunza kupitia kwao jinsi nchi zingine zinavyoendesha siasa zao zaidi ya hapo hamna jingine? Diaspora walio na umuhimu kwa hii nchi ni wanaotuma pesa nyumbani kusaidia familia zao na sio wanaoshabikia siasa.
 
Hawa Diaspora wanaoambiwa wa-download tibisii app na Ryoba. Wewe umekimbia huku Bongo kwenye dhiki umeenda kwenye mkate na wine alafu unakuja kuimbishwa salam maria ya Kalamaganda.

Tatizo ni kwamba ukianzisha siasa dhidi ya serikali yako NA una hatihati ya kupoteza uraia na haki zotee. Chance ya kuwa mkimbizi ni kubwa ni kama dada yetu Mange Kimambi.
 
Kwa kweli ni wazo zuri kutumia diaspora kuleta mabadiliko. Hasa kwenye sekta ya elimu na afya.RC wa Dar anaweza kutusaidia jinsi alivyoweza ku mobilise wana diaspora wa Marekani mpaka waliweza kutoa kontena 38 kwaajili ya sekta ya elimu.
 
Unafiki,Uoga,Ubinafsi, Wizi, Ujivuni, Maneno meeengi hizo ndio sifa ambazo karibia kila mtanzania anazo hata azaliwe na kukulia Newyork pale kama ni mtanzania lazima awe na hizo sifa, Watanzania tuliowengi ndio tuko hivyo.

Ndio maana utajiuliza sana inakuaje Watanzania kila mahali tunakwama, kwenye sports hatumo, kwenye uchumi hatumo, kwenye siasa hatumo, kwenye elimu hatumo, kwenye teknolojia hatumo, kwenye kila kitu na kila siku tunakwama.
 
Kwa jinsi walivokuwa wanamshangilia Kabundi kwa maneno yake yaliyojaa uongo, seems hawafuatilii yanayoendelea Tz
 
Mkuu unaweza kutuwekea vivutio vya uwekezaji kwa wana diaspora. Si wengi wenye tsarina hizi.
 
Sidhan mkuu.. Mimi hata kurud tz naogopa. Mwanangu ananbembeleza akamjue mama yake Na nchi yake Namwambia baba kule hakufai. Na akil zangu zlivyo watanidaka air port. Mimi nilitaka nianzishe vita ya mtandaon na hii serikali bado ninawaza najiona kama musa.

Ntakayewakomboa wana wa israel. Bado nnawaza sana hivi hekalu walilolibomoa kwa miaka 60. Hivi ntaweza kulijenga kwa miaka minne ... Nnawaza mkuu
 
Usijidanganye rafiki yangu Tanzania kuna nafasi nyingi za kufanya maendeleo , watu wanafanya maendeleo tena makubwa sana kuliko hata waliopo Ulaya . Watu wanajenga , wanafanya kazi za utalii. Wewe kaa huko halafu uje utajikuta umechelewa.Cha msingi ni kushughulisha kichwa chako na usijiingize kwenye vitu vya kukupotezea muda kama siasa utapata mafanikio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…