JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Kuhamasisha wananchi kuhusu vita dhidi ya umaskini ni moja kati ya wajibu wa Diwani.
Katika kulitekeleza hili ni lazima ajue kwa ufasaha hali ya kiuchumi na kijamii inayowakabili wananchi wake na kushirikiana nao ili kupanga mipango endelevu ya kujikwamua.
Vile vile ana wajibu wa kufuatilia utekelezaji wa mipango yote ya wananchi na ya Halmashauri.
Ili kutimiza jukumu hili ipasavyo, Diwani anatakiwa kufuatilia utekelezaji wa miradi yote ndani ya Kata yake ambalo ni jimbo lake la uchaguzi bila kudai malipo yoyote toka kwenye Halmashauri au wadau wengine. Kimsingi hii ndiyo kazi ambayo Diwani aliahidi kuitekeleza wakati wa kampeni.
Upvote
0