Je DPP wa Tanzania Anawajibika Kwa Watanzania au wachache waliopo Madarakani?

Je DPP wa Tanzania Anawajibika Kwa Watanzania au wachache waliopo Madarakani?

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
3,978
Reaction score
6,739
Ni kitu cha kwaida kuona kuwa mfumo wa kisheria wa nchi yoyote, mchakato wa haki na uwajibikaji ni msingi muhimu wa utawala bora.
images - 2025-02-28T212906.062.jpeg

Hapo ndipo tunapozungumzia, nguvu na mamlaka ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ambayo ni sehemu ya muhimu katika kuhakikisha kuwa haki inapatikana bila upendeleo. Lakini ndani ya Tanzania haswa upande wa Tanganyika, kuna maswali kadhaa yamepata kuumiza watu vichwa, yanajitokeza.

Je Mkurugenzi huyu anatekeleza wajibu wake kwa maslahi ya wananchi wote au anatekeleza maagizo ya wanasiasa au watu wachache wenye ushawishi mkubwa katika serikali?
images - 2025-02-28T213002.913.jpeg


Katika mfumo wa kisheria wa Tanzania, Mkurugenzi wa Mashtaka ana jukumu la kuongoza na kusimamia mashtaka ya jinai katika mahakama. Hii inamaanisha kwamba yeye ni kiungo muhimu katika kuhakikisha kuwa haki inatendeka kwa watu wote. Lakini swali linaloumiza watu vichwa ni:

je, Mkurugenzi huyu ni mtekelezaji wa sheria kwa manufaa ya Watanzania kama taifa zima au anakuwa na upendeleo kwa kundi fulani la watu?.

Mamlaka ya DPP na Uhusiano Wake na Serikali.
images - 2025-02-28T212945.083.jpeg


Kama ilivyo katika nchi nyingi, DPP nchini Tanzania ni nafasi ya kitaifa na inategemea ufanisi wake katika kutekeleza majukumu ya haki. Hata hivyo, DPP huteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, jambo ambalo linaweza kutoa taswira kwamba nafasi hii inaweza kuwa chini ya ushawishi wa serikali.
images - 2025-02-28T212906.062.jpeg


Ikiwa Rais au viongozi wa serikali watakuwa na maslahi fulani katika mashtaka yanayoendelea, kuna hatari ya kuwa DPP ataingiliwa katika mchakato wa kuchagua ni nani atakayeshtakiwa na nani atapewa msamaha.

Mara kadhaa tumepata kuona baadhi ya watu wakisota mahabusu na kesi zao kupigwa tarehe kila uchwao, miezi na hata miaka na tunakuja kushtuka kusikia kauli ya DPP kuwa hana tena nia ya kuendelea na kesi hivyo mtu huy awe huru? Je msimamo huu wa DPP unakuwa ni kwa manufaa ya watanzania ama manufaa ya watu wachache?

Je, DPP Anatekeleza Haki ya Kisheria au Maagizo ya wakuu wake?
images - 2025-02-28T213002.913.jpeg


Mkurugenzi wa Mashtaka anapochukua hatua ya kuwashtaki watu fulani au kuachilia wengine, je, anazingatia ukweli na ushahidi ulio mbele yake, au anashinikizwa na viongozi wa kisiasa? Chama? Kundi la watu wenye nguvu? Ama ushawishi upi?

Hii ni swali linalozua wasiwasi miongoni mwa watanzania wenye utimamu. Ikiwa DPP atakuwa akitekeleza maagizo kutoka kwa Rais au viongozi wa serikali, basi mfumo wa haki unaweza kudhoofika kwa kiasi kikubwa sana, na haki inaweza kuwa siyo kwa wote, achilia mbali watanzania kwa ujumla.
images - 2025-02-28T213046.559.jpeg


Kuanzia mwaka 2020 mpaka sasa, kuna mifano mingi sana ambayo iliibua maswali kuhusu mchakato wa kushughulikia kesi kubwa za ufisadi na utawala. Hali hii iliwafanya wananchi wengi kujiuliza kama DPP alifanya maamuzi kwa uwazi, kwa manufaa ya umma, au kama alikuwapo kutekeleza maelekezo kutoka kwa serikali ama Rais.
images (3).png


Hali hii inaendelea kuleta mjadala mkubwa kuwa, je DPP ni taasisi inayojitegemea katika kutenda haki au kama ni sehemu ya mkakati wa serikali ama chama?.

Uwajibikaji wa DPP kwa Wananchi wa Tanzania.

Katika demokrasia, ni muhimu kwa Mkurugenzi wa Mashtaka kuwa na uhuru na uwezo wa kufanya maamuzi bila kuingiliwa na wanasiasa au mamlaka yoyote. Hii inatoa uhakika kwa wananchi kwamba mashtaka yanayowasilishwa mahakamani yanasimamia haki, siyo maslahi ya kundi fulani ama watu wachache.
images - 2025-02-28T213202.902.jpeg


Ni ngumu sana na inatia ukakasi kuona namna ambavyo DPP anaendesha mashtaka kwa nguvu kubwa na baadaye kudai kuwa hana nia ya kuendelea na shauri hilo, sidhani kama hili jambo ni kwa ajili ya afya ya watanzania.

Kama kweli Mkurugenzi wa Mashtaka anawajibika kwa watanzania na anatekeleza majukumu yake kwa kutenda haki, basi anapaswa kuwa na uhuru kamili wa kufanya maamuzi bila kuingiliwa na serikali au watu wenye ushawishi mkubwa.
images - 2025-02-28T212906.062.jpeg


Ni katika hali hii itamsaidia kudumisha imani ya wtanzania katika mfumo wa sheria. Ikiwa DPP atakuwa akifanya kazi kwa manufaa ya viongozi wa kisiasa pekee, basi haki itakuwa imekosekana, na mamlaka ya DPP yatakuwa yamepoteza maana yake ya kuwa mlinzi wa sheria kwa watanzania wote.
images - 2025-02-28T212945.083.jpeg


Kumsumbua mtanzania miezi mpaka miaka akiingia viunga vya Mahakama ya Kisutu kisa tu ana mawazo tofauti na Rais, ama Waziri Mkuu sio suala ambalo DPP unapaswa kuunga mkono kabsa ili wakuu wapate kufurahi.

SLYVESTER MWAKITALU NI MTUMISHI WA UMMA, NI MTUMISHI KWA AJILI YA WATANZANIA WOTE! HAUPO JUU YA SHERIA! WEWE NI MSAADA KWA WATANZANIA! FAHAMU HILO.
images - 2025-02-28T212906.062.jpeg
 
Back
Top Bottom