Nilichosikia na kushuhudia ni kwamba Jonathan Mbwambo bado hajamaliza PhD. Anasema kuwa iko katika hatua za mwisho kabisa kwa external examiner. Unajua PhD inawezekana kuwa supervisors wako (mara nyingi wawili) wanaweza kuwa wameridhika na kazi yako: lkn kwa utaratibu wa vyuo vyote, lazima kuundwe external PhD committee ambayo itasoma kazi nzima, kuutisha "defense" na kutoa verdict. Sasa nilichosikia ni kuwa huyu jamaa amekwama hapo; ameshindwa kumshawishi mmoja wa examiner kuwa amefanya vizuri utafiti wake, hasa upande wa methodology. Haya ni mambo ya kawaida kwa PhD, mana unakuwa hujui unamaliza lini: Issue yangu kubwa hapa ni KWANINI TAYARI ANATUMIA TITLE YA KUITWA DOCTOR (Dr)?????...Anataka kumpendezesha nani? Hilo naamini kabisa Prof Kuzilwa analijua...mana ni mshikaji wake sana: Kuzilwa hana uwezo wa kumkemea, ni kiongozi dhaifu pmj na kuwa Academic Credentials zake hazina wasiwasi.
Tungependa Mzumbe University watoe Press Release Kuhusu Hili; mana ni sawasawa na mtu kujiita Advocate na kwenda vijijini na kuwadanganya wanakijiji kuwa atawasaidia katika kupitia kampuni yake kwenye matatizo yake ya Ardhi...Huu ni udanganyifu....
Napenda mtoe michango yenu katika hili...hasa wanafunzi wa wote wa Mzumbe hasa wa Dar Campus...