IsayaMwita
JF-Expert Member
- Mar 9, 2008
- 1,127
- 140
ndiyo, ushindi dhidi ya ccm utakuwepo. tatizo ni kwamba hatafanya hivyo...sijui ni kwasababu ya vyeo, au mbowe unajua mimi huwa sielewi ni kitu gani kinamzuia?
Mpeni sifa Yesu
Unamaanisha kwamba CCM (Kikwete) atashinda au?
IsayaMwita,
Mwacheni Dr. Slaa aendelee kugombea ubunge huko Karatu maana hana uwezo wa kumshinda Kikwete. Sio kwamba hana sifa au hafai, hapana, tatizo ni chama chake ambacho hakijafika vijijini na pia CCM wakitumia mabavu yao hasa kwa wananchi wa vijijini, itakuwa ngumu sana kwa Dr. Slaa hata kupata asilimia 30 ya kura.
Kuliko kumpoteza huyu mpiganaji, ni bora aendelee kuendeleza mapambano kule bungeni. Ninaamini hata Slaa analijua hilo na kafanya maamuzi mazuri ya kuendelea kubaki bungeni.
ashinde kwa kura zipi achana na watanzania wamelogwa na ccm
ndiyo kikwete atashinda. ila tukimweka Dr.slaa kwenye vyama vya upinzani, kikwete atashindwa....tatizo ni kwamba, Dr.slaa hatakubali kugombea urais, sijui tatizo lake ni nini wakati watu kibao wana tumaini juu yake. au hajiamini?
muheza2007
Ukija Dar niletee Machungwa toka pale segera, ndugu yangu umeongea naye Dr Slaa
Sawa IsaMwita. Ila machungwa yetu yanaoza kwasababu ya kukosa viwanda huku Dar mnanunua juice za kuchanganya madawa kutoka SA.
Hawa CCM wamerogwa sijui ugonjwa gani. Huku Tanga tumebahatika na kiwanda cha maziwa na kinasaidia sana wananchi wafugaji ingawaje bei yao ndio inaua kabisa, lakini nafuu angalau hayaozi majumbani.
Mpeni sifa Yesu
Ndugu yangu huu utabili wako mbona umekuwa haulidhishi, na tena hauna mshiko Mkuu?
haulidhishi kivipi mkuu, na kivipi hauna mshiko, unamaana watz hawamkubali Dr. au? silaha ya ufisadi ni tosha kabisa kuidondosha ccm kama awareness ikipelekwa vijijini kwa njia za mikutano, kwa njia za vipindi vya radio, kwanjia mbalimbali....na Dr angepita...hivi unafikiri Lipumba kwa mfano mwingine... na usomi wake ule, akama angekuwa anakubalika na watu wengi, si tungeshashinda...lakini watu baadhi wanaogopa ile sera yake ya ngunguli, jino kwa jino na watu wanaoandamana kuwa wengi wao wamevaa kanzu...isingekuwa hivyo, nakwambia ccm ni raisi sana kuing'oa either kwa njia ya CHADEMA au kwa njia ya CUF. siku iyo ipo tena inakuja mbioooo
Labda jambo lisilofahamika ni kuwa watanzania hawamchagui mtu kwa umaarufu. Pia, matokeo ya washindi kwenye uchaguzi ambayo yanatangazwa si lazima yawe yanayotokana na kura zilizopigwa. Therefore, there is no way Slaa anaweza kumsinda Kikwete, especially kwa uchaguzi wa mwaka huu
usipende kusema twafa sema nafa , mwache mzee wa watu akawapiganie wananchi wake wa karatu mageuzi nchini bado kitendawili mifumo ya kusimamia chaguzi haijatulia hivyo upinzani kutangzwa washindi si rahisi . Nenda zako karatu mzee/ laa
Dr. Slaa hawezi kushinda ikiwa wewe na wengine wote hamtampa kura zenu...Lakini Chadema na Dr.Slaa kama chama watakuwa wametimiza wajibu wao kumsimamisha mtu ambaye anaweza kuweka upinzani na kuiongoza nchi kwa sababu nyingi za msingi.
Dr.Slaa anazo sifa za - Opposition Leadership ambazo huanza na Tabia kuwa ni pamoja na 1. stubbornness na disagreeableness pale pasipokuwa na haki pasipo kupoteza loyalty to his superior.
2. He is Visionary na assertiveness 3. Tender minded - with great concern for the less fortunate 4. Hardworking na persistent 5. Open minded 6. Attentive to his emotions 7. Imaginative 8. Exceptional ability to tolerate stress and adversity, and many many more one can think of....
Yote haya tumeyaona hapa JF..Mungu atupe nini zaidi jamani, gunia la chawa?
Mtu yeyote mgombea aliyeshindwa kusimama na kuukosoa Utawala wenye mapungufu au makosa ya wazi hawezi kuwa Great President. Sii swala la sisi kujiuliza umaarufu wake auanaweza kutuongoza ila sisi kumuomba mtu huyu asimame dhidi ya JK kwa sababu tunamhitaji. Na hata kama atashindwa uchaguzi mkuu bado atakuwa ametimiza wajibu wake mkubwa tokana na sifa alizokuwa nazo, kazi itakuwa kwetu sisi WAJINGA sio yeye tena..
.