Je, Economy Driver Company sio matapeli?

Je, Economy Driver Company sio matapeli?

Omuzaile

Member
Joined
Jan 23, 2019
Posts
34
Reaction score
56
Habari Wana jamii forum, ningependa kujua kuhusu hawa watu je sio matapeli? Kwa hapa Kibaha maili moja wapo ukumbi unaitwa mwitongo, kwakweli Wana wanafunzi wengi mno haswa kutoka mikoa jirani, nilimuhoji mwanafunzi mmoja kuhusu utaratibu wao ndo akaniambia ukiwa unaanza unaambiwa mafunzo ni bure Ila tu form ya kujiunga ndo elfu 20 utajitegemea malazi ndo utajitegemea tu,

Ila walishangaa walipofikisha mwezi mmoja waliambiwa walipe laki 6 ili waweze kuendelea hatua inayofuata.
Na wanaahidiwa wakimaliza watawapatia ajira pamoja na kiwaunganisha kwenye makampuni yao.

Je, serikali haswa hapa Kibaha wanaijua hii kampuni, please kama unajua chochote kuhusu hawa watu share nasi tuweze kuwaokoa hawa wadogo zetu kwa kuliwa hela pia kupotezewa muda.

ASANTE.
 
Sijui chochote kuhusu hiyo kampuni Ila kwa maelezo y'ako mafupi hao ni matapeli.

Wanatapeliwa hao
 
"hao mpaka waseme na watasema" akili ni nywele mtu wangu
 
Back
Top Bottom