Je,elimu unayoisoma inatija mbeleni katika maisha yako?

bomouwa

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2014
Posts
1,149
Reaction score
800
Wanajf habari zenu?
Nafahamu humu wengi ni wasomi na pia wameelimika vyakutosha kiasi ambacho kinawawezesha waishi maishi ama wayapendayo ama wasioyapenda.
Vijana wengi wamekua wakifanaya maamuzi juu ya mustakabali wao wa elimu hasa pale wanapoanza kuchagua combinations wafikapo kidato cha tatu na pia inawajengea msingi wakutimiza ndoto zao wanapohitimu o level na kuanza safari ya A level ili kujikita zaidi katika masomo aliochagua. Sasa tatzo linakuja pale ambapo kijana amemaliza na anakosa kufahamu ni kwanini ameamua kuchagua kitivo fulani katika elimu ya juu?je, anamatarajio sawa na hali halisi ilivyo?soko la ajira linahitaji kitu anachochagua?

hayo ni maswali ambayo yanawafanya vijana wengi wakose ajira katika soko kwa kua wamekua na elimu ambazo katika soko la ajira hazina mahitaji kuwatosheleza wote. Pengine vijana wengi hapa ndipo wanapokosea mpaka kufanya taifa kua na wasomi wengi ambao hawana uwezo wa kutumia taaluma zao kujiendeshea maisha yao wenyewe.
Kuna mtu alituma post yenye kicha cha habari "nina degree ya archeology natafuta ajira/nitajiajiri vipi?"

sasa katika hali ya kawaida unaweza kuona kabisa mtu huyu alisoma kitu ambacho hakujiuliza maswali muhimu kabla ya kufikia uamuzi wa yeye kuingia darasani, angalia mtu anasoma degree ya tourism and hospitality(ieleweke ni mfano na siwadharau graduates hawa) sasa soko la utalii limewekezwa na wawekezaji ambao wanamahoteli na wanahitaji faida sasa hapa kunatofauti kati ya mfanyakazi aliepata degree hiyo ndani ya kazi na yule fresh graduate kuanza kuomba kazi na ndo maana unaona vyuo vya mijini kama datastar,intel na vinginevyo vya type hiyo ndivyo vinavyopata soko kwakua viajana wanaosoma ngazi ya certificate ambazo hazitambuliki nacte wanakua wanahitajika kwa kazi za mahotel maana anaweza kutandika kitanda,kufanya usafi room, kuhudumia wageni vinywaji n.k kitu ambacho graduate hawezi maana anafanya degree akiwa na mawazo ya kuja kua manager katika secta ya utalii.
ukiangalia graduates wenye degree za wildlife management wengi walio tanapa, ngorongoro na idara ya wanyamapori sio fresh from school bali ni watumishi waliojiendeleza wakiwa makazini, sasa hii inajenga picha kua vijana wanakosa elimu juu ya kufanya maamuzi sahihi katika kuamua mustakabali wa maisha ya mbeleni.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU BARIKI VIJANA WA TANZANIA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…