Je, Elimu ya Msingi na Sekondari zimeondolewa TAMISEMI?

Midimay

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2015
Posts
3,036
Reaction score
5,039
Habari za jioni wana JF?

Kuna kitu katika teuzi na reshuffle za jana ambacho naona media na wana social media hawajaweza kukikamata( ku capture).

Kitu chenyewe ni uteuzi wa Naibu Katibu Mkuu Dr. Franklin Rwezimula kwenda WEST(wizara ya elimu, sayansi na teknolojia) kushughulikia elimu ya Msingi na Sekondari.

Kabla ya hapo Elimu za Msingi na Sekondari kwa maana ya Operations, Human Resource na Miundo Mbinu ilikuwa TAMISEMI toka mwaka 2008.

Sasa huu uteuzi wa jana umenichanganya kidogo na bahati mbaya sijaweza kufuatilia uapisho kama Mazaa amesema neno lolote juu ya hilo.

Kama ni kweli, basi namuunga mkono katika hilo. Mambo yote ya elimu yabaki katika wizara ya Elimu. Kama ni mahitaji kule chini, basi capacity ijengwe huko huko ndani ya WEST.
 
Lakini katika WEST kuna idara ya ElimuMsingi ambayo inaratibu maswala yote ya kisera kwa shule za Msingi na Sekondari nchini.

Kama ambavyo kuna Sehemu ya Mafunzo ya Ualimu, Elimu Maalumu na Uthibiti Ubora wa Shule na Vyuo (vya Ualimu) katika WEST
 
Hakuna kilichoondolewa wala kukatwa, nadhani watu ni wengi wanaotakiwa kuteuliwa so hizo nafasi zinatanuliwa ili kamba izidi kulefuka!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…