Je, FedEx wana ofisi pale airport Dar? Kuna anaefahamu mizigo ya FedEx inafikia ofisi ipi Kwa ajili ya custom clearance

NoFvcknName

Member
Joined
Oct 21, 2021
Posts
6
Reaction score
8
Kuna mzigo wangu(laptop) umefika Dar Kwa kutumia FedEx, Mimi npo Dom (na nililipa Pesa ya na nauli na kuweka address ya Dom). Lakin naona mzigo umefika upo customs, ila wamenipigia simu ili kufanya mchakato wa kufanya clearance, lakini bado wanataka Pesa nyingine 118000(Kwa ajil ya kufanya clearance), na nkiangalia vizur naona si kampuni ya FedEx, ni kampuni nyingine inaitwa Faris Express Services Company ndo wanataka hio Pesa. Je

1. Inakuaje wanakua na gharama hivo kutoa mzigo. Nilishawahi tumia DHL gharama zao ni 0.6% ya bei ya mzigo
2. Kutoa laptop airport ni lazima agent naweza kwenda mwenyew?
3. Kama agent ni lazima kwanin wasifanye FedEx wenyewe, wawape watu WA Kati wenye gharama hiv.

Naombeni ufafanuz zaid labda kuna vitu sivifahamu hapa
 
Hakuna Fedex Tanzania so lazima hao ni maagent. Clearing kufanya mwenyewe ni ngumu. Kampuni nyingi za usafirishaji hawasemagi bei kamili mzigo ukifika ndio unashangaa unatakiwa kulipia VAT mara TBS.
 
FedEx wako Mikocheni Chato Street.

Pesa wanayohitaji nadhani ni ya malipo ya uwakala wa forodha na Sio ushuru.

Lakuzingatia katika manunuzi kuna namna ya kuchagua kulipia mzigo wako plus usafiri na gharama za forodha toka huko mzigo unakotoka. Na hii mara nyingi ndio wanafanya DHL. Hizo kampuni nyingine utaona cheap sana ila mzigo ukishafika ndio gharama kama hivi Sasa.

Asante.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante sana Kwa michango yenu wadau, mana nilishawahi tumia huduma za DHL, aisee hawa jamaa wako very professional na on time, na gharama nafuu(at least Kwa mizigo nilio agizaga) hawakua na Kona Kona nyingi kama hawa FedEx, clearance charges zao nafuu sana(mbali na customs fee) na wanafanya wenyew sio watu WA Kati.

Ndo mana hawa FedEx wamenish2a kidogo na hii michanganuo yao
 
Sitakuja kutumia FEDEX Tanzania maisha yangu yote. Kwanza imechukua zaidi ya mwezi mzigo kutoka airport alafu local charges zao zipo juu sana. Wanachelewesha makusudi unakutana na gharama za storage. Mzigo nilinunua $35 marekani. Ila gharama za hapa imeshafika 300,000 plus mpaka sasa hivi. Bora DHL wako professional sana na hawana hidden fees zozote
 
Pole Sana ndugu, hawa jamaa wanajivuta Sana, na sidhan Kama ni rafiki Kwa mizigo midogo. Ila pia nilishawahi tumia USPS (shirika la posta la marekani) gharama ni za kawaida sana, na mizigo inakuja mpaka pale posta Dar, kama ni ushuru utamaliza pale, na mara nyingi mizigo midogo hulipi hata hela(au wanaweza Pima tu kwny mzani, alafu unalipa hela ndogo Sana).
 
Mi mzigo ulipofika tz walinichaji gharama za documents toka ofisini kwao kama 88k then wakaniambia kama Nina agent wakunifanyia clearance Basi aende akachukue doc ili aweze kuendelea na clearance
 
Nilikuwa nafanya mchakato niagize simu toka south korea kupitia hawa jamaa, sasa mbona mnanitisha tena?
 
sitakuja watumia hawa FEDeX TZ tena, learned by mistake
Mkuu unaweza kunisaidia mawasiliano yao fedex tz
Kuna mzigo wangu(laptop) umefika Dar Kwa kutumia FedEx, Mimi npo Dom (na nililipa Pesa ya na nauli na kuweka address ya Dom). Lakin naona mzigo umefika upo customs, ila wamenipigia simu ili kufanya mchakato wa kufanya clearance, lakini bado wanataka Pesa nyingine 118000(Kwa ajil ya kufanya clearance), na nkiangalia vizur naona si kampuni ya FedEx, ni kampuni nyingine inaitwa Faris Express Services Company ndo wanataka hio Pesa. Je

1. Inakuaje wanakua na gharama hivo kutoa mzigo. Nilishawahi tumia DHL gharama zao ni 0.6% ya bei ya mzigo
2. Kutoa laptop airport ni lazima agent naweza kwenda mwenyew?
3. Kama agent ni lazima kwanin wasifanye FedEx wenyewe, wawape watu WA Kati wenye gharama hiv.

Naombeni ufafanuz zaid labda kuna vitu sivifahamu hapa
Mkuu unaweza kunisaidia mawasiliano ya fedex tz, namba yao iliyoko mtandaoni naona hawapokei
 
Mkuu unaweza kunisaidia mawasiliano yao fedex tz

Mkuu unaweza kunisaidia mawasiliano ya fedex tz, namba yao iliyoko mtandaoni naona hawapokei
Nimekutumia pm. Ila kama uko dar nakushauri uende physically.ni wagumu kujibu email au kupokea simu
 
Back
Top Bottom