Je, forever living ni scams??

talentbrain

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2009
Posts
1,187
Reaction score
760
Niwasalim wajuvi wa mambo na wale tusiojua juu ya hili tutafaidaka na msaada wa wenye ujuzi juu ya hili.

Kwa siku kadhaa nimekuwa nikipigiwa, tumiwa sms na kuelezwa juu ya kujiunga na Forever Living Products {FLP} na kwamba waliojiunga na bishara kupitia company hii wamefanikiwa na wengi waliokuwa wameajiriwa wamejiajiri na kuacha kazi za kuajiriwa. Wamekuwa na mafanikio makubwa ndani ya vipindi vifupi na kwamba wamekuwa wakisafiri nje mara kwa mara.

Habari za mafanikio zilinitisha na kuanza kutilia shaka juu ya kuwepo na upatu au scams katika biashara hii. Nikaona si vema nikatae au nikubali kujiunga na biashara hii kabla sijaja hapa kuuliza kwa wanye ufahamu na au wameshafanya suala hili.

Ukweli ni kwamba sijawahi kumuona mtu aliyefanikiwa kwa biashara hii, japo sikatai kuwa hakuna waliofanikiwa. Ila nataka nipate ithibati na ushuhuda ambao utaondoa shaka niliyonayo.

Nimejaribu kufuatilia juu ya hili na kukutana na mjadala huu ambao uliongeza hofu yangu. Pitia hapa: Is Forever Living Products a scam? should I beocme a seller? - marketing | Ask MetaFilter


Watanzania wenzangu na wahangaikaji kama mimi nipeni maelezo juu ya kitu hiki pia iwasaidie watu wengine.
 
Mkuu ni vyema ukatafuta information sahihi kabla hujajiunga
 
Mkuu hio kitu sio scam ni network marketing kama ilivyo GNLD, TIANSHI, n.k. ila tofautisha na wezi kina Telexfree ambao sana sana main product yao ni kuuza membership hence Ponzi / Pyramid Scheme.

Network marketing unapata faida kwa kusajiri watu na commission kwa kazi ya uliyowasajiri wakisajiri au kutumia products, hence utaona hapa kuna movements ya products fulani ambazo watu inabidi watumie/wanunue ili wewe upate faida

Katika ugumu au urahisi au ujiunge au usijiunge jaribu kuangalia hapa nilitoa uzi kuhusu ugumu na changamoto za network marketing Tanzania

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...matatizo-ya-network-marketing-tanzania-2.html
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…