Je, form 34A na 34B ni nini?.... Hizi hapa!

issac77

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2013
Posts
4,128
Reaction score
7,899
Kukataliwa kwa matokeo ya uchaguzi katika tovuti ya tume ya uchaguzi nchini Kenya kwa mara nyengine tena kumezua majina ya fomu zinazotumiwa katika kunakili matokeo ya uchaguzi.

Fomu zilizotajwa na mgombea wa upinzani wa Nasa Raila Odinga ni zile za 34A na 34B.

Katika kuyakataa matokeo hayo ya IEBC katika mtandao wake bwana Odinga alisema kuwa fomu 34A na 34B lazima zitolewe.

IEBC imesema kuwa maajenti wa mgombea huyo wa urais wataonyeshwa fomu 34A.

Je hizi ni fomu gani?

Chini ya sheria ya uchaguzi, fomu 34A ndio fomu ya kwanza inayotumika kunakili matokeo ya uchaguzi wa urais.

Fomu hiyo hujazwa na afisa wa tume ye uchaguzi anayesimamia uchaguzi huo kwa jina la Presiding officer baada ya kuhesabiwa kwa kura katika kituo cha kupigia kura.

Fomu hiyo huwa na maelezo kuhusu kura zilizohesabiwa za kila mgombea mbali na kuwa na idadi ya wapiga kura katika kituo hicho, kura zilizoharibika, zile zilizo na utata na kura zilizokubalika.

Mgombea ama ajenti wake baadaye hutakiwa kutia saini ili kuthibitisha kwamba yaliomo ndani ya fomu hiyo ni sahihi.

Kifungu cha 39 cha uchaguzi kinasema kuwa ili kufanyika kwa uchaguzi wa urais tume ya uchaguzi itatoa matokeo hayo kielektroniki baadaye kuyasafirisha kutoka katika kituo cha kupigia kura hadi katika kituo cha kuhesabia kura cha eneo bunge na baadaye katika kituo cha kitaifa cha kuhesabia kura.
 
Fomu hizi ndizo zilinyamazisha chadema na lowasa wao Tanzania waliposema wameibiwa waliulizwa kituo kipi fomu hizi hapa wakaufyata hadi leo. Tume ya uchaguzi kenya hizo fomu.ndizo.zaweza maliza tuhuma sio matokeo ya komputa.tume ianike hadharani fomu zote za matokeo kila kituo
 
Dikteta kamponza mwenzako. Majimbo yote ya umasaini yaliyokuwa ngome ya Raila yameenda kwa Uhuru kazi ya Lowassa imelipa.Uhuru umasaini kashinda kwa zaidi ya sabini na tano asilimia jambo ambalo hajawahi kuliota.
 
Dikteta kamponza mwenzako. Majimbo yote ya umasaini yaliyokuwa ngome ya Raila yameenda kwa Uhuru kazi ya Lowassa imelipa.Uhuru umasaini kashinda kwa zaidi ya sabini na tano asilimia jambo ambalo hajawahi kuliota.
Mbona Lowassa naye ni dikteta kwani kwenye utawala wake wakurugenzi walikuwa wakimwogopa kwa kitendo cha kuwafukuzisha kazi hovyo hovyo, hivyo walifanya kazi kwa woga. Mmesahau shule za kata zilijengwa kwa babe kuliko leo?
Halafu kama siyo umburura unajisikiaje kumuunga mkono mgombea Rais nchi nyingine akashinda, Hivi utajidaije wakati kwetu hamuwezi?
 
Watu wanafikiri wamesahau,nakumbuka wakati wanajenga barabara ya shekilango alimtukana mkuu wa mkoa mbele ya hadhara wakati huo mzee makamba kama mtoto mdogo

ploudly ngosha [emoji243][emoji243][emoji243]
 
Hueleweki, bila kumtaja Lowasa unawa. Shwa
 
Huyo Lowassa alikuwaje dikteta? Kweli unajua maana ya dikteta? Dikteta anayelazimishwa kujiuzulu? Unaweza tu kuwa dikteta kama unavyo vyombo vya kutekeleza maamuzi yako na hivyo vyombo vinawajibika kwako na si kwa mwingine. Huwezi kuwa dikteta huku dola haiko chini yako...huu upumbavu mnautoa wapi? Je Lowassa amewahi kuwa Rais wa nchi hii? Je amewahi kuwa kiongozi mkuu wa chama tawala? Amewahi kuwa Jemadari Mkuu wa vyombo vya usalama? Amewahi kuwa na kinga dhidi ya mashtaka? Mgambilwa ni mntu, yawezekana unajua kuandika lakini hujaelimika hata chembe.
 
Udikteta mkubwa ni kula mali ya nchi na kujilimbikizia mali kiujanjaujanja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…