Je, gari yenye engine capacity chini ya cc 1000 inafaa kwa safari ndefu?

Nsaji wa Lila

Senior Member
Joined
Feb 1, 2021
Posts
118
Reaction score
152
Wakuu kwema?

Hivi gari ya cc 990 na cc 1290, zina tofauti gani kwenye suala la kupiga masafa marefu?

Maana wengine wanasema kama gari engine capacity yake ni ndogo huwezi kwenda nalo masafa marefu kama Dar to Kagera bila kuweka vituo vingi katikati.

Je, hili lina ukweli?
 
- Inaweza safari?, Ndio.

- Zingatia taratibu zake, kwakuwa unaelewa uwezo wa gari husika.
Maana sijawahi kwenda masafa marefu na gari chini ya cc 1490.

Ila kuna jamaa yangu ameenda hadi Bukoba kwa vitz ile ya cc990, hapo breki ya kwanza, Dom, kisha Misigiri, then Nzega, halafu Kahama, Chato then katoboa Bukoba.

Sasa naona vituo ni vingi sana, na mie napenda nikianza safari iwe moja kwa moja.
 
Kama pikipiki tena yenye air-cooler inaenda itashindwaje gari yenye rejeta?

Sema kama alivosema mdau Mwl.RCT hapo juu, ushajua gari yangu haiwezi shindana na wenye 2.0L zingatia haya:

1. Take it slow. Kama unahitajika uko "masafa marefu" mapema ni bora ukaondoka siku moja kabla kuliko kukimbizana njiani.

2. Jiwekee vituo kadhaa. Mfano kila baada ya 80-100km au 2 hours of driving itategemea pana mji au centre pumzika. Simamisha gari. Pata msosi afu zunguka zunguka ufanye utalii.

3. Ifanyie service kabla haujaondoka. Especially ya Oil, matairi, breki, etc.

4. Usibebe mizigo kupiliza. Ushajua gari yako haina cc kubwa so na nguvu (hp) itakua ndogo, usijibebee mizigo utaitesa. Mfano ukataka ule vichwa njiani lets say 3, pia ukabeba na mazawadi mazawadi unaweza ona una save kumbe unalitesa gari.

5. Mkiwa wawili itakua poa. Kupokezana maana hiyo safari ni ndefu.

6. Obey sheria zote ili kupunguza gharama za kuwatoa toa trafick.

Kwa experience yangu mimi nishaenda na IST Mbeya na Dodoma nishaipeleka Passo kwa mteja.
 
So kwa uzoefu wako, kwa hiyo cc990 unatoboa hadi mbeya?? Bila vituo vituo??
Bila vituo ndio ila why taking risk. Dar to Mbeya kilometa 800 hizo bora ubreak kila baada ya 200. Mfano Moro, Iringa, hafu Makambako au ukamalizia.

Uzuri ukivuka Moro uko kuna baridi sana so cooling itakua more effective.
 
Mkuu kwa Passo zipo zenye engine chini ya CC 1000 alkadhalika Vitz. Vipo nyingine zenye engine ya piston tatu lakin hizi gari ni town Cruiser zimeundwa kwa wale watuamiji wa mijini mtuajia anae endesha gari chini ya km 70 wastani kwa siku. Lakini zinaweza pia kwenda mbali kama vipo na services nzuri lakini kwa masafa ya mara kwa mara huuu mkuu mwezi tu linakua borongoto.
 
Ni kweli mkuu, sasa mfano kila baada ya miezi minne unaenda Arusha from Dar au Mbeya. But most of time unakuwa Dar, je haifai kuitumia kuendea huko mkoani??
 
Hizo gari we unazoita town cruizer we nzio ndo wanapiga nazo masafa mf.unakuta mtu ana ist, vits anaanzisha ligi na mtu wa Subaru Forester hapo yuko highway hajui kuwa anaua gari mdogo mdogo, TRA mnatukosea sana kwa huo ushuru watz tunashindwa kuendesha ndinga za maana kwa sabb yenu, watu wanakalia kununua vits, ist, Porter n.k
 
Ni kweli mkuu, sasa mfano kila baada ya miez minne unaenda arusha from dar, au mbeya. But most of time unakuwa dar, je haifai kuitumia kuendea huko mkoani??
Mkuu inafaa kabisa. Sema inabidi uijali utumie quality oil na service ontime maana vipuri vyake vinaaribika mapema. Sema kaa ukijua hizo Gari siyo za masafa marefu hata ukisafiri nayo mbali utagundua unachoka sana pamoja na ni automatic ukilinganisha na SUV mfano Prado.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…