Je hapa kuna ukweli

Enny

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
962
Reaction score
130
Kuna dada yangu yupo katika ndoa kwa miaka nane sasa hajabahatika kupata mtoto. Amehangaika kwenye mahospitali mengi na mpaka alishafanyiwa operation ya mirija kwani walisema mirija yake imeziba.

sasa juzi katika kusoma gazeti akakutana na tangazo linalosema Tiba za kisayansi kutoka UK. kama nilivyoambatanisha hapo. wao wanasema wana dawa za kuzibua mirija bila operation na kutibu matatizo ya uzazi.

Mwenye kuwajua hawa watu tafadhari naomba msaada maana sitaki aende kupoteza hela bure.
 
alishafanyiwa operation ya mirija ...wana dawa za kuzibua mirija bila operation
sasa kiongozi kama alishafanyiwa operation hizo dawa tena za nini,au operation haikuwa na mafanikio?
 
Ukweli unaweza ukawepo maana sayansi zinazidiana, lakini kwenye kuzibua mirija naona asirudie tena maana kama ulivosema keshafanyiwa operation lakini haikuzaa matunda so kama atatutumia dawa iwe ni kwa ajili ya matatizo mengine ya uzazi
 
Wajaribu kutofanya mapenzi two weeks kabla ya tarehe zenyewe za kushika mimba. Pia Male awe anakula vyakula vya protein kwa wingi na Female aepuke vyakula vya mafuta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…