Je, Harmonize anaanza kupotea?

Youngstunna

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2016
Posts
266
Reaction score
300
Habarini waungwana poleni na majukumu?

Moja kwa moja niende kwenye mada kama ilivyo tajwa hapo juu ,Waswahili wanasema mshika mawili moja humponyoka je hivi ndivyo ndugu yetu harmonize hatakavyo ponyokwa na muziki kwa kuingilia siasa.

Sio jambo baya kwa mtu kuwa na upande wake (chama cha siasa) anachounga mkono ila si vyema kwa msanii kama yeye kujionesha hadharani tena kwa kupitia jina ku sapoti siasa fulani kinamna moja naona kama hii itagawa sana mashabiki wake, au ndo anajipigia kampeni chini kwa chini ili awe muheshimiwa.

Kiukweli hajazungumza jambo baya na yote aliozungumza ni ukweli, ila sidhani kama hii ni vyema kwa msanii kama yeye maana atagawa mashabiki zake na sio lazima kila msanii mkubwa mwenye influence awe mbunge, Ubunge ni cheo na pia nidhama na nikipaji pia mimi nadhani konde boy anapaswa kufanya muziki siasa hawaachie wanasiasa mfano mzuri ni kwa king kiba

Professor J yeye alikuwa mwanaharakati tokea mwanzoni hata ukisikiliza mashairi yake kwenye ndio mzee unajua dhahiri huyu ana siasa ndani yake lakini sio kwa harmonize atapotea

Nawasilisha.
 
Jiulize marangapi unaambiwa umekosea wakat uoni kama umekosea kuna maisha kabla ya ivyo vitu
 

Clouds, wcb wana support na hata wanamuziki wao kuimba siasa

Kesho Mond atatoa nae wa ccm

Kama una akili sahihi, ni demokrasia pia

Na hawatapotea

Himiza wa chadema nao waimbe!!!!!!

Otherwise, tulia subiri mfungue shule ukaendelee kujifunza hesabu za log
 
Sipingi kuwa na demokrasia lakini siasa na muziki haviendani wasanii wengi wa Tz wanajikomba na hivyo ndivyo hugawa mashabiki.Tafadhali endelea kuangalia tamthilia ya sultan kwa shemeji yako.
 
iyo kawaida,, mbona hata kala Jeremiah katoa wimbo wa mapambio.
Dogo anaangalia fursa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…