Bango moja limetuletea maana mpya ya mapinduzi kuwa ni kutokata tamaa!!!kwani nani katika CCM ana dalili ya kukata tamaa na nini kimesababisha hali hiyo?
Hivi mapinduzi si tulisoma kuwa ni mabadiliko ya ghalfa katika nyanja za kisiasa,kiuchumi kijamii na kiutamaduni yanaoendeshwa na, kwa faida ya tabaka tawaliwa?
Ningependa kusikia Nape amemweleza huyo bibi na wenzake kuwa yeye,alipata nafasi ya kuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa ,mwaka 2002,akiwa na miaka 24 tu ,wakati huo bado akisoma Chuo cha Siasa Kivukoni katika ngazi ya CHETI (CERTIFICATE) na wala si chuo kikuu!!
Sijui wangejiskiaje hao wanamapinduzi wasiokata tamaa.utashangaa wao wanaota vyeo!!!
Kuna bango linataka serikali iwachukulie hatua wakosoaji wa CCM na serikali!!!
Wanajua idadi ya waajiriwa wa serikali wanoichukia CCM & serikali?
Hizo hatua zikianza kuchukuliwa wapo tayari kukabiliana na matokeo yake ?
Wanajua kama UDSM ndio palipo na wahadhiri wanaoikosoa serikali ipasavyo?
Wanajua kuwa wahadhiri wa pale kila leo wanalia kuhusu 'Uhuru wa Taaluma'na kuwa walisikitishwa na sakata la kumnyima Baregu mkataba mwaka 2010.Wanajua kuwa hata kada mwenzao, Dtk Benson Bana alisononeshwa na hatua hiyo?
Wanajua kuwa madhara ya pendekezo lao hilo la kitoto?