Je haya mashirika ya haki za wanawake na ukatili wa kijinsia yapo kweli? Ukatili na dhuluma ya haki kwa mwanamke huyu

Je haya mashirika ya haki za wanawake na ukatili wa kijinsia yapo kweli? Ukatili na dhuluma ya haki kwa mwanamke huyu

Hell2Heaven

Senior Member
Joined
Mar 3, 2021
Posts
173
Reaction score
465
Ulisha ona maajabu ya ukatili wakijinsia alafu polisi wana mpooza mke kwa kumpa elfu 50 eti akapike ili yule polisi aje kusuluishia kesi nyumba jioni?

Hii imetokea moshi mjini kituo cha mjini standi, ambapo mwanamke anaye nyanyaswa kikatili na mume wake kwa vipigo vilivyopelekea mimba 3 kutoka, vipigo vya kichwani, vipogo vya kung'atwa ulimi, vipigo vya mateke ya tumbo na kukanyagiwa shingo chini nusu ya kufa,kukimbizwa uchi wa mnyama usiku bila hata chupi, na hatimaye kipigo cha mwaka huu kilicho pitiliza miaka yote 12 ya unyanusaji ya kumvunja mtu pua na akalazwa na kufanyiwa ct-scan na doctor kudhibitisha puwa na jicho kuathirika ndani.

Polisi wa dawati la jinsia ndiye aliye tuma mtu hadi hospital alipo lazwa muadhirika..Nandiye aliye muita mume polisi na akaja kudhaminiwa kwa milioni moja.. Baada ya hapo wakati mwanake ana ambiwa arudi siku kadhaa mbele ili afung
Liwe jalada la kwenda mahakamani..

Ghafla siku anaenda mkuu wa kituo ana muita ndani aki mkaripia kuwa huja pigwa na na kanusha hadi vipimo vya doctor ambaye wenyewe walimpa pf3 akaenda kutibiwa na waka mhoji akiwa kitandani.. Na baadaye alipotoka hospitali wakampa rb ya mume mushikwa lakin ajabu . Polisi hao hao walio mwambia huyu mama aende akapewe jalada wapeleke kesi mahakamani..


Siku inafika mwanamke anafika kituoni amabiwa hujawahi kupigwa na mke ana lia kwa uchungu mbele yake roho, kwa aibu ana mpa eti elfu 50 aende nyumban akapike ili huyo polisi aje jioni kusuluisha..

Hii ina nisikitisha maana huyu mwanamke amkekuwa akitoa taarifa za kupigwa polisi mara kwa mara ziaid ya mara 4, achilia mbali. Hayo mengine yaliyo ishia kwa wasuluishi wa kifamilia zaidi ya mara 12,

Mtu ana athiriia kisaikolojia, kiafya kimwili, na hata kiuzalishaji kwa kufanyiwa fujo hadi kazin kwake na mume kuapia kuwa ana wajua maasikari wa moshi wote hivyo aende popote hawata msaidia..

Ana apia kuwa ndoa haivunjiki mpaka amue au yeye afe. Ajabu mume huyu alisha rudishiwa mahari na wakwe zake..Na akaipokea, lakin ameshupalia kuwa yeye ame oa kiroman katholik hivyo ana haki ya kupigia na kufanya chochote..

Mwanamke alisha toka kwa mume mara 4, na kwenda kupangisha kivyake lakin mume amekuwa akimfanyia fujo kazini na hata katika makazi yake.. Na baadaye humrudisha kwa nguvu nyumbani.

Naombeni wanao jua hawa wanao jita mashirika ya watetezi wa haki za binadamu na ukatili wa kijinsia watupe namba ili niwaonganishe na muhusika hali yake siyo nzuri ana umizwa sana.

Kumbuka mimi na wewe ndio tutafanya mabadiliko ya kuifanya jamii yetu iwe sehemu ya usawa na amani.

Asanten
Nashindwa kuweka namba zake hapa ilanikipata watu sahihi nita waonganisha na muadhirika.
 
Zipo Ila zimekaa kutegeshea pesa ya msaada.
Mchangieni atafute wakili mzuri afungue kesi mahakamani pia ajaribu kumwona mkuu wa mkoa au wilaya awaripoti polisi au atumie hata vyombo vya habari.
 
Back
Top Bottom