Walker Water
JF-Expert Member
- Aug 23, 2022
- 842
- 3,357
Leo naomba tuangalie na kujiuliza na kujijibu baadhi ya maswali yanayoonekana kuwatatiza watu wengi.
1. Mimi ni nani?; Mimi ni nafsi, mwili na roho.
2. Nimetoka wapi?; Nimetoka kwa Mungu Mkuu.
3. Amenileta kufanya nini hapa duniani?; Kufanya kazi yake ya kipekee ambayo hakuna mwingine ataweza kuifanya hapa duniani.
4. Nitaijuaje hiyo kazi?; Nitamuuliza yeye aliyenileta.
5. Nitamuulizaje?; Natafuta sehemu tulivu ya peke yangu na yeye nikiwa na kalamu na daftari kisha namwambia rohoni kuwa ninakikao na wewe na ninaomba unijibu haya maswali yangu, hakika ananijibu.
6. Kwa mimi nisiyeamini habari za Mungu na shetani nafanikiwaje?; Nimeumbwa kamili, hivyo najiwekea malengo yangu na ninatumia hekima yangu ya kibinadamu na nguvu zangu na ninafanikiwa kama nilivyopanga. Niwe mwaminifu tu.
7. Kwa nini Mungu asimuue shetani kabisa ili niishi kwa raha?; Hiyo kazi yote ameniachia mimi, yeye ananipa tu nguvu, hivyo mimi ndiye mwamuzi wa mwisho wa nini nimfanye shetani ( nikimwonea huruma sawa!).
8. Kwa nini Mungu aniumbe bila makubaliano yangu; Hapana, aliponiumba aliniuliza kwanza nikutume duniani ukafanye hichi na hichi, nikakubali mwenyewe, nikatolewa ufahamu nikazaliwa duniani na siku nazaliwa Mungu nilimwona akinipokea na siku ya kufa pia nitamwona dakika za mwisho ndipo nife. ( Sitapona nikishamwona ili nisije nikasimulia anafananaje).
9. Kwa nini nikifanya dhambi atanichoma pamoja na shetani?; Kwa sababu nimeumbwa kamili na nilivyofika duniani nikaacha kufanya kilichonileta nikaungana na shetani na kupendana naye na nimpaka nikiri mwenyewe kuwa nipo tayari kuchomwa naye na Mungu yeye ndiye mwonevu na hana haki.
10. Nifanyeje nitekeleze mambo yangu hapa duniani ili niishi kwa raha na kufa?; Nachagua kutekeleza mipango ya Mungu au yangu binafsi au ya shetani,yoyote kwa bidii. Mungu na shetani mipango yao ili ifanikiwe hapa duniani lazima wamtumie binadamu kwa sababu ana mwili. Mimi na vyote na hivyo naweza kutekeleza ya kati yao au yangu binafsi.
Karibuni wadau kwa maswali mengine, maswali na majibu au kuuliza swali na jibu lenye utata kati ya haya niliyo yaorodhesha