Je, Hayati Magufuli alichukia wawekezaji au alichukia wawekezaji janja janja?

Nenda kaombe kazi ya kufundisha kiingereza Kenya Kwa sabbu unaweza kuandika kiingereza fasaha kuliko wakenya ulete mrejesho hapa!
 


MAGUFULI ALIKUWA HATABIRIKI UNAWEZA UKALETA MTAJI MKUBWA HALAFU AKAWATUMA KINA DOTTO JAMES KUJA KUIKWAPUA HUKO BENKI
 
Huelewi chochote kuhusu sarakasi za ikulu kati ya jpm na huyo mwenzake..kojoa ulale hujui chochoteee
 
JPM aliipenda Tanzania kwa dhati kabisa. Wanaomchukia ni wale waliotaka na wanaotaka kunufaika binafsi na Tanzania badala ya kuinufaisha Tanzania. Binafsi nitaendelea kumuenzi JPM daima na kuililia Mama Tanzania hadi mwisho wa uhai wangu!
 
Rubbish!
 
Kuna watu munajisema semea kila kitu hata mambo ya hovyo hovyo! Hii lugha ya wako vizuri umeitoa wapi? Au wakikuzidi wewe unasema wako vizuri? Nchi gani duniani yenye watu wako vizuri na nyingine wako vibaya? Ubora, quality, ni juu yako siyo juu ya utaifa na nchi. Kazana nawe uwazidi wenzako, wakenya na wa-TZ badala ya maneno ya kusifia bila sababu.

Ubora wautoe wapi? Shuleni? Shule zao ni nzuri kuliko zetu? Yes au NO! Ni nzuri ktk nyanja zipi? Zote? Yes au No! Mbona hatuoni ugunduzi wowote wa Kenya? Mbona hatuoni dalili za ufahamu? Wewe inabidi tukufundishe hata kufikiri.
 
Limekuingia na umeumia sana. Pole lakini ndiyo ukweli. Haya nazungumzia kutokana na experince na siyo bla bla. Endelea kukasirika kwani sina msaada zaidi.
 
Rubbish vipi tena? Kasema ukweli. Wabongo siyo kiswahili siyo kiingereza kote apeche alulu. Ukisoma michango ya hapa JF uone maneno ya kiswahili yanavyoandikwa utabaki unasikitika. Tulikosea wapi jamani.
 
Unawezaje ukaruhusu walimu wa Kenya nchini wakati tuna maelfu wa wahitimu wa Kitanzania wanaotaka hizo ajira?

Hizi ndizo akili za wanachama wa chama cha mbowe!
Walimu wa kiswahili duniani kote wanatoka kenya,hata watangazaji wa channel za kimataifa za kiswahili wanatoka kenya.Kuongea kiswahili sio ndo kujua kiswahili
 
Kwa kuangalia jinsi uwekezaji katika shule za English medium has a mikoa ya Ars, K'njaro na Manyara, ni kweli kabisa naungana na hoja hii maana nimeshuhudia kwa macho yangu. Brother yangu mm alikuwa Meneger was shule ya mwekeza mama mmoja kutoka Australia, hii shule hadi Leo IPO maeneo ya USA-RIVER jirani kabisa na hotel ya Ngurdoto. Sikh nilipopata nafasi ya kumtembelea nilishangaa sana kukuta staff yenye walimu 60 wakenye ni wengi kuliko watanzania. Wakati Luna shule nyingine za namna hiyohiyo zikiwa na walimu watanzania lkn bado zina ufanisi sawia. Hili suala LA hawa wakenya lazima tuwe makini sana
 
Mfu shetani mtu Magufuli alikuwa anataka mwekezaji atakayekubali kufanya naye ufisadi vinginevyo anakufilisi na kukufungulia kesi ya kutakatisha fedha na uhujumu uchumi!
Acha utoto wa majukwaa ya kisiasa. Hapa tunajadili mambo serious ya nchi na kujenga akili. Nani aliyefilisiwa unayeweza kumsifu ni mtu mwaminifu. Ukizoea misheni tauni, kina kitu cha hovyo unaona ni halali yako.
 
Hao walimu toka Kenya wameajiriwa wakati wa SSH au wakati wa JIWE?
 
Walimu wa kiswahili duniani kote wanatoka kenya,hata watangazaji wa channel za kimataifa za kiswahili wanatoka kenya.Kuongea kiswahili sio ndo kujua kiswahili
Ni kwa sababu umezubaa zubaa kama mbumbumbu ndio maana wakenya wanakupiku.

Badala ya kuchangamkia fursa umelala tu kwenye kochi unajamba na kusifu juhudi za wengine.

Changamka!
 
Ila kiswahili kigumu kaka, wengine tulipata D O-Level na janja janja zetu..
 
mwandazake alikua na huluka na tabia zake zinazomfaa yeye kama yeye tu na hazielezeki.
 
Hii ilipata wapi? Story hii wanaijua wazee wachache (ambao bado wanaishi) wa pale Kashalunga, Muleba mahali familia ya akina Magufuli ilikoishi hadi robo ya kwanza ya 1960s, kisha kuamua Biharamulo na baadaye Kyato!
Hii ndiyo kazi ya JF, ukijifanya mjuaji watu wanakufunyua. Mwendazake alikuwa na tabia zisizofanana na Watanzania, ilibidi tuchimbe ndiyo tikajuwa ana asili ya Burundi
 
Uongooo
 
Limekuingia na umeumia sana. Pole lakini ndiyo ukweli. Haya nazungumzia kutokana na experince na siyo bla bla. Endelea kukasirika kwani sina msaada zaidi.
Experience ni relative kwa mazingira yako.
Sema bhla! bhla! siyo bla bla. Nikishaona hilo najua ndo sababu unasifia hao!
 
Labda tuseme sisi ishu ni kutojiamini. Nina mdogo wangu amepata fursa ujerumani anafundisha Kiswahili na alikuwa mwalimu tu wa kawaida sekondari. Ni kwamba tuwe na uthubutu. Nishawahi muuliza Expatriate mmoja kwa nn hamtuchukui na sisi nchini kwenu kama Expatriate. Jibu lilikuwa stereotype, kwamba watanzania hatupendi kufanya kz nje ya TZ. Hivyo inawezekana stereotypes kuhusu watz ndo zinatuwekea vigingi. Siyo kila mtanzania mvivu, mswahili au mbabaishaji.
 
Kuwachukia kunasaidia nini kama nchi haina wenye uwezo huo? Kama Kenya imeweza kuwajengea uwezo watu wako na ujasiri wa kutoka kutafuta kwingine Tanzania tunaendekeza sifa za siasa uchwara lazima watufunike.

Kuongea kiswahili huku kitaani na mitandaoni haimaanishi tunaweza kukifundisha. Kufundisha na kuongea tuu vitu viwili tofauti.

Ujamaa umeliharibu sana taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…