Je hii inawezekana au ni uzushi mtupu?

merick david

Member
Joined
Jul 19, 2011
Posts
17
Reaction score
10
Eti kuna habari kwamba watu wakiishi katika mahusiano ya kimapenzi muda mrefu sana huanza kufanana katika mambo mbalimbali kam vile sura na tabia je ni kweli au uzushi?. karibuni sana wanajamii tujadili ili tupate ukweli
 
Kimsingi hakuna ukweli katika hilo,hata mkae kwa muda mrefu kiasi gani haitakaa itokee mfanane sura,kidogo labda tabia kwa sababu mwenza wako,mmoja wenu atajaribu ku'cope' na mwenzake ili walau wafanane,mfano kwenda baa,disko,outing,nk
 
Eti kuna habari kwamba watu wakiishi katika mahusiano ya kimapenzi muda mrefu sana huanza kufanana katika mambo mbalimbali kam vile sura na tabia je ni kweli au uzushi?. karibuni sana wanajamii tujadili ili tupate ukweli

Ni kweli kabisa, hususan namna ya kuongea, namna ya kuji express, namna ya kusikiliza, namna ya kukaripia, na tabia nyingi tu hufanana. Talking from experience, ni mara kadhaa watu wameni-confuse kuwa ni ndugu na Gozi langu, hatuhusiani ndee wala sikio, tuna miaka 30 pamoja!
 
Tofautisha kufanana na kuigana, mlichofanya wewe na Gozi lako ni kuigana vijitabia vyenu katu hamuwezi kufanana.
 
Tofautisha kufanana na kuigana, mlichofanya wewe na Gozi lako ni kuigana vijitabia vyenu katu hamuwezi kufanana.

Hii ni kitu ambacho hata mimi sikioni lakini wale wanaonifananisha mara kwa mara ndio wanaonipa "notion" ya kuwa tunafanana. Unajuwa mkianza kufana tabia, namna ya kuongea, namna ya kucheka na kuigana, kuna kauwezekano kakubwa sana hata sura mkaanza kufanana.

Kuna research ilifanywa, nikiipata ntakuwekea, waliwekwa watu na wake zao, wanaume wotw upande mmoja na wanawake wote upande mmoja, wakaitwa watu wasijuana nao kabisa wachague mtu na mkewe, kati ya wanandoa wote walioishi zaidi ya miaka 15. 90% walipatia.
 
Duh kumbe wee ni kijeba namna hiyo??? Ndio maana mara zote mada zako unazochangia ni za upogoupogo tu. Kumbe ni kibibi????? Sikamooo bibi!!!!!!!!!!!
 
Kweli ndugu halia ubishi ktk tabia ila sura mh uhakika sina
 
msisahau baada ya kula keki sasa wamekuwa mwili mmoja sasa mwashangaa nini kama tabia zao zimeshabihiana?
 
Duh kumbe wee ni kijeba namna hiyo??? Ndio maana mara zote mada zako unazochangia ni za upogoupogo tu. Kumbe ni kibibi????? Sikamooo bibi!!!!!!!!!!!

Marahaba mjukuu, na uanze kuniwekea heshima yangu kuanzia sasa.
 
Eti kuna habari kwamba watu wakiishi katika mahusiano ya kimapenzi muda mrefu sana huanza kufanana katika mambo mbalimbali kam vile sura na tabia je ni kweli au uzushi?. karibuni sana wanajamii tujadili ili tupate ukweli
Mbona kiranja wa mawaziri wetu kakiuka hili?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…