rantheb
Member
- Jun 27, 2018
- 86
- 45
*SERIKALI KUWAPATIA VITAMBULISHO WAKULIMA*
Baada ya Serikali nchini Tanzania kugawa vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo 675,000, sasa inahamia kwa wakulima ambao nao watapatiwa vitambulisho na kusajiliwa.
Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano Januari 2, 2019 mjini Dodoma na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga.
Amesema tayari taratibu zote zimekamilika na kinachotakiwa ni kuanza kazi ya kuwatambua na kuwasajili ili Serikali iweze kutambua idadi ya wakulima na uwezo wao wa kuzalisha.
Amesema mpango huo utasaidia wakulima kupata masoko ya mazao yao na nchi kujua ina kiasi gani cha chakula kwa ajili ya watu wake.
Kwa mujibu wa Hasunga, usajili huo utafanyika chini ya Wizara hiyo na bodi za mazao ambao wameelekezwa kutowabagua wakulima, kuhakikisha wanaosajiliwa ni wakulima.
“Katika hili tutataka kujua huyu mtu analima shamba lenye ukubwa wa kiasi gani na liko wapi, je anatarajia kuvuna kiasi gani katika msimu unaokuja,” amesema Hasunga.
Kuhusu gharama za vitambulisho, amesema Wizara inaacha jambo hilo kwa bodi za mazao, kwamba havitakuwa na bei kubwa.
“Hapana si kwamba tunarudisha kodi kwa mgongo wa nyuma, kinachofanyika ni kuwatambua na hizo gharama za vitambulisho hazitakuwa kubwa,” amesema Hasunga.
Chanzo: Mwananchi
Kama ni kweli itaathiri mambo yafuatayo!
1. Uzalishaji wa mazao utapungua mno, kwa sababu kigezo cha kupewa kitambulisho atii ni shamba..... Je kwa wale wanaokodisha mashamba itakuwaje?
2. Itashusha uchumi kwa kiwango kikubwa
.....maana sio tu wenye mashamba ndio wakulima!
3. Itaongeza waharifu, kwa vijana wa mjini ambao wanakodi mashamba na kulima kijijini wakikosa vitambulisho vya mkulima kisa hawana mashamba hali itakuwa mbaya sana.
Sent using Jamii Forums mobile app